Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Tuesday, February 21, 2017

Serikali na wadau kujadili ufaulu kidato 2

WIZARA ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imesema itakutana na wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili kuhusu pendekezo la kupandishwa kwa wastani wa ufaulu kidato cha pili kutoka wastani wa asilimia 30 uliopo sasa hadi asilimia 40.
Hayo yamesemwa na Kaimu Kamishna wa Elimu katika wizara hiyo, Nicholaus Burreta wakati alipofanya mazungumzo na gazeti hili.
Kauli ya Burreta imekuja baada ya Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii(CSSC) kueleza kwamba ili kuhakikisha kuwa kuna sera, sheria, viwango na miongozo ambayo inatengeneza mazingira mazuri ya kupanua na kuboresha utoaji wa elimu, itaanzisha mazungumzo na serikali ya kupandisha alama ya wastani ya ufaulu ya kidato cha pili kutoka silimia 30 hadi 40 ili kuboresha elimu.
Burreta alisema suala la kupandisha ufaulu sio la wizara pekee, bali ni lazima kushirikisha wadau mbalimbali ili kuona kama kwa hali hiyo ya sasa wanaweza kuongeza kiwango cha ufaulu au waendelee na kiwango kilichopo.
“Tunatakiwa tukae tutulie tushirikishe wadau kama hao waliosema wanataka tuzungumze ili tuone namna gani ya kutekeleza suala hili ni wazo zuri wametoa, lakini tukae tuone ni kwanini tuliweka kiwango kilichopo na tuone ni kwanini tufike mahali tubadilishe kiwango bila kuathiri mfumo wa elimu,” alieleza Burreta.
Alisema suala la taaluma ni suala linalotakiwa ushirikishwaji wa kutosha ili lisilete malalamiko na bila kuathiri ubora wa elimu unaotolewa nchini hivyo kwa kuwa wazo hili limetoka katika kundi moja watakaa na wadau wengine kuchukua mawazo yao kuhusu kwa nini wapandishe na baadaye watatoa taarifa kwa umma.

0 comments:

Post a Comment