Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa (wa
kwanza kulia), Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge
wa Mkuranga Abdallah Ulega wakivuta kamba kwa pamoja kuashiria ufunguzi
rasmi wa kiwanda cha kusindika Matunda cha Bakhresa Mwandege mkoani
Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa
wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kiwanda hicho cha usindikaji wa
matunda kilichopo Mwandege mkoani Pwani. Wengine katika picha ni
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Bw. abubakar Bakhresa, Mkuu wa mkoa wa
Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega na
Waziri wa Viwanda Biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Mtendaji Mkuu
wa Bakhressa Food Products Salim Aziz Salim.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
na Mwenyekiti wa Kundi la Makampuni ya Bakhressa Said Salim Bakhresa
wakiangalia mojawapo za hatua za usindikaji wa matunda aina ya maembe
katika kiwanda hicho kilichopo Mwandege mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na wafanyakazi Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya
kufungua rasmi kiwanda cha Usindikaji wa Matunda cha Bakhresa kilichopo
Mwandege mkoani Pwani.
0 comments:
Post a Comment