Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Monday, May 22, 2017

Trump apania kusuluhisha mgogoro wa Israel na Palestina


Rais wa Marekani baada ya kumaliza ziara yake suadi arabia leo ameanza ziara yake ukanda wa nchi za Mashariki ya kati ambapo ameanza taratibu za kuketi pamoja na viongozi wa nchi ya Israel na Palestina Bw Trump anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi wa Israel na Palestina katika kipindi cha siku mbili atakazokuwa eneo hilo. Rais huyo amesema kupatikana kwa mkataba wa amani kati ya Waisraeli na Wapalestina yatakuwa mafanikio makubwa, lakini hakusema mkataba kama huo unafaa kuchukua mwelekeo gani. Amesema angependa sana pande zote mbili ziamue kuhusu mkataba huo wa amana kwa mashauriano ya moja kwa moja. Katika mkutano mkuu wa viongozi wa Kiislamu na Kiarabu mjini Rihadh siku ya Jumapili, Bw Trump aliwataka viongozi hao kuwa kwenye mstari wa mbele katika kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu na wapiganaji wenye itikadi kali na "kuwafurusha kutoka kwenye dunia hii." Aliitaja moja kwa moja Iran na kusema kwamba imekuwa "ikichochea mizozo ya kidini na ugaidi" katika kanda hiyo kwa miongo mingi. Bw Trump pia alikariri tena kwamba anaamini amani kati ya Waisraeli na Wapalestina inaweza kupatikana. Rais huyo wa Marekani amekuwa akichukuliwa sana kuwa muungaji mkono mkubwa wa Israel kuliko mtangulizi wake Barack Obama. Amechukua msimamo usio mkali kuhusu suala tata la Israel kujenga makazi ya walowezi maeneo ya Wapalestina na kudokeza kwamba upanuzi wa makao hayo na si kuwepo kwa makao yenyewe, unaweza kuwa ndio kikwazo katika kutafuta amani. Zaidi ya Wayahudi 600,000 huishi katika makao makazi 140 ya walowezi ambayo yamejengwa tangu Israel ilipotwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem mwaka 1967, maeneo ambayo Wapalestina huyachukuliwa kuwa sehemu ya "taifa litakaloundwa" la Wapalestina. Makazi hayo ni haramu chini ya sheria za kimataifa, lakini Israel hupinga hilo. Rais huyo pia ametoa ishara za kukanganya kuhusu mji wa Jerusalem, na kuahidi kuhamishia ubalozi wa Israel mjini humo kutoka Tel Aviv, hatua iliyowakera Wapalestina lakini ikawafurahisha sana Waisraeli. Hata hivyo, baadaye alionekana kulegeza msimamo huo, na Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson majuzi aliambia NBC News kwamba Bw Trump bado analitafakari jambo hilo

Friday, March 24, 2017

Runinga Ya Kidini Yachezasha Video Ya Ngono

Runinga ya Touba nchini Senegal
Runinga moja ya kidini nchini Senegal imemlaumu mtu mmoja ambaye hakutajwa kwa hujuma ya kishetani iliosababisha kanda moja ya ngono kuonyeshwa hewani.
Watazamaji wa runinga ya Touba walishangazwa wakati picha hizo za ngono zilipoonekana katika runinga zao kati ya saa saba na dakika kumi na saa saba unusu siku ya Jumatatu.
Runinga hiyo ya kibinafsi awali ilikuwa imesema kuwa kulikuwa na tatizo la mitambo lililosababisha tatizo hilo.
Runinga ya Touba inaendeshwa na kundi la Waislamu kutoka Senegal la Mouride.
Chombo hicho sasa kimewasilisha malalamishi yake kwa mamlaka ili kuwasaka wahusika.
Video hiyo ya ngono ilichezeshwa wakati wa kipindi maarufu cha Tarixu Juma kwa takriban dakika 15.
''Kama chombo cha kidini, usimamizi wa Touba TV pamoja na watazamaji wake wameshangazwa na wanashtumu kitendo hiki cha kihalifu ambacho kinaonekana kuwa hujuma za kishetani dhidi ya chombo kinachojulikana kwa kupigania maadili ya kiislamu na mafunzo yake'' ,ulisema usimamizi wa Touba TV
Runinga hiyo inapeperusha vipindi vya kidini na kukuza maadili ya kiislamu na mafunzo yake.
Haijulikani ni vipi washukiwa waliweza kuingia katika mitambo ya runinga hiyo.
Touba ndio runinga ya pekee ya mji wa madhehebu ya Mouride, ambayo ina ushawishi mkubwa wa kisiasa pamoja na kiuchumi nchini Senegal.

Wanahabari Watatu Wauawa Ndani Ya Mwezi Huu Mexico

Ujumbe ulioachwa baada ya kuuawa kwa Mirosalva Breach umeonyesha wauaji walichukizwa na Ripoti zake
Muandishi wa habari nchini Mexico ameuawa kwa kupigwa risasi katika jimbo la Chihuahua, yeye ni mwana habari wa tatu kuuawa nchini humo mwezi huu.
Mirosalva Breach alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake nje ya makazi yake mjini Chihuahua.
Mmoja wa watoto wake ambaye alikuwa naye ndani ya gari, hakujeruhiwa.
Watu wenye silaha waliacha ujumbe uliosema '' kwa kuwa na mdomo mrefu''.
Bi Breach aliripoti kuhusu masuala ya uhalifu, biashara ya dawa za kulevya na rushwa katika gazeti la kitaifa, mjini humo La Jordana na Notre de Juarez.
Kamati inayotetea waandishi wa Habari imesema wanahabari 38 wameuawa nchini Mexico tangu 1992.

Thursday, March 23, 2017

Wyclef Jean ashukiwa kimakosa kuwa mwizi Los Angeles

Mwanamuziki Wyclef Jean amewalaumu polisi huko Los Angeles, Marekani, kwa kumshuku kuwa mwanamume ambaye aliiba kutoka kituoa cha mafuta kilichokuwa karibu.
Mwanamuziki huyo raia wa Haiti, alichapisha video yake kwenye mtandao wa twitter akisimama karibu la gari la polisi baada ya kufungwa pingu.
Alidai kuwa polisi wa Los Angeles walimfunga pingu bila ya sababu yoyote lakini idara hiyo ya polisi ilikana kufanya hivyo.
Wyclef Jean anafahamika vyema kuwa moja wa waanzilishi wa kundi la rap la Fugees na ameshirikiana na wanamuzi kama Shakira, Timbaland na Lil' Kim.
Anasema alikuwa kwenye sudio na mwanamuziki T-Baby wakati kituo cha mafuta kilipopowa, na kudai kuwa alisimamishwa na polisi baadaye kwa sababu alikuwa mtu mweusi ambaye alikuwa amefunga bandana iliyokuwa ikifanana na mtu aliyepora kituoa cha mafuta.
Akiongea na BBC msemaji wa idara ya polisi wa Los Angeles alisema kuwa Wyclef Jean, alikuwa kwenye kiti cha abiria kwenye gari lililokuwa likifanana na lile lilotumika kwenye wizi.
Polisi walisema kuwa walimwachilia bila ya kumfungulia mashtaka.

Tuesday, March 21, 2017

Alichokiandika Rais wa Benki ya Dunia kuhusu jiji la Dar es salaam

Baada ya kuwekwa jiwe la msingi kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu (interchange) katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam March 20, 2017 kwa ufadhili wa Bank ya Dunia, Rais wa Bank hiyo Jim Yong Kim ameandika haya kuhusu jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla.
“Kama ilivyo miji mingi ya Afrika, Dar es Salaam uliopo Tanzania unakua kwa haraka – na hivyo ni mji wenye msongamano wa magari. Suluhisho linahitajika, hivyo nilipewa heshima kujumuika na Rais John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya barabara ya juu Ubungo.
‘Sehemu hii ya miundombinu itawaunganisha watu wengi kwenye kazi na nafasi mbalimbali na kufanya safari kwa mabasi mapya ya mwendokasi. BRT imeelezwa kuwa tayari imepunguza muda wa kusafiri kwa dakika 90. Bank ya Dunia inafurahi kuunga mkono kazi zote na inaangalia mbele kusaidia kulifukia pengo la miundombinu Tanzania na kwingineko Afrika.” – Jim Yong Kim.

Waasi Washambulia Tena Damascus

Vikosi vya waasi na wapiganaji wa Jihad nchini Syria vimesema kuwa shambulio la hivi karibuni walilotekeleza mjini Damascus, kubwa zaidi kutokea katika kipindi cha miaka miwili ,linapeleka ujumbe kwa serikali siku kadhaa kabla ya awamu nyingine ya mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kuanza mjini Geneva.
Wapiganaji wamesema shambulio hilo lililotokea umbali wa chini ya kilometa tatu kutoka mji wa kihistoria Damascus, unaonyesha kuwa bado wana uwezo wa kufanya shambulizi kubwa katika mji ambao unaelezwa kuwa na ulinzi mkali.
Kuhusu mkutano huo mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amesema pande zote zimethibitisha kuwa zitashiriki kwenye mazungumzo hayo

Waziri Ajiuzuru Nchini Ufaransa

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa,Bruno Le Roux, amejiuzulu, baada ya kuibuka shutuma kuwa aliwaajiri binti zake wawili kuwa wasaidizi wa bunge wakiwa wanafunzi.
Waendesha mashtaka walifanya uchunguzi wa awali kuhusu mikataba yenye thamani ya karibu dola elfu sitini ambazo bwana Le Roux aliwapa binti zake kati ya mwaka 2009 na mwaka 2016.
Amesema hakuna sheria ya bunge iliyokiukwa na watoto wake walifanya kazi kwa uhalali, lakini hakutaka kuwa kikwazo kwa Serikali.
Wakati huohuo, uchunguzi kama huo umeendelea kufanyika dhidi ya mgombea urais kutoka chama cha Conservative Francois Fillon, ambaye anashutumiwa kufanya udanganyifu.
Fillon amekana kuajiri familia yake na kuwalipa mishahara minono, kashfa ambayo imetia dosari mchakato wake wa kuwania urais

Monday, March 20, 2017

Sekta Ya Nyama Yaingia Matatani Nchini Brazil

Rais wa Brazil, Michel Temer, amezihakikishia nchi za kigeni kuwa , kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, haina maana kuwa bidhaa zake si salama.
Rais Temer amewaambia mabalozi kuwa nchi yake bado imeendelea kuzalisha nyama yenye ubora, ingawa kumekuwa na shutuma kuwa viwanda vyake vikubwa vitatu vimekuwa vikiuza nyama iliyooza kwa miaka mingi.
Serikali ya Brazil ina wasiwasi kuwa Marekani, China na nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kupiga marufuku kuingiza nyama kutoka Brazil baada ya shutuma hizo za kushtua zilizojitokeza siku ya Ijumaa.
Polisi nchini humo walifanya ukaguzi nchi nzima na kushutumu makampuni ya ufungaji nyama JBS, BRF na makapuni mengine madogo madogo kwa kuuza nyama isiyo salama, kuku na bidhaa nyingine za nyama.
Zaidi ya wafanyakazi 30 wa serikali waliokuwa na jukumu la kukagua vitendo hivyo wanachunguzwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Mhandisi aliyepewa jina Saddam Hussain akosa kazi

Ni zaidi ya miaka kumi sasa tangu kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa Iraq Saddam Hussein ambaye ingawa alipingwa sana na baadhi ya watu, alipendwa sana na wengine.
Saddam ameendelea kuathiri maisha ya watu, hasa waliopewa jina lake.
Mmoja aliyeathirika ni mhandisi wa masuala ya baharini Saddam Hussain ambaye alipewa jina hilo na babu yake miaka 25 iliyopita Saddam Hussein alipokuwa bado ni maarufu.
Lakini Hussain ametatizika sana kutafuta kazi, jambo ambalo anaamini linatokana na jina lake, ingawa kuna tofauti kidogo kwamba anaitwa Hussain badala ya Hussein.
Anasema ametafuta kazi mara 40 bila mafanikio.
Kwa sasa, amewasilisha kesi mahakamani kujaribu kubadili jina lake awe akiitwa sasa Sajid.
Shughuli hiyo hata hivyo ilichukua muda mrefu.
Saddam Hussain alifuzu kutoka chuo kikuu cha Noorul Islam, Tamil Nadu miaka miwili iliyopita.
Yeye ni mzaliwa wa Jamshedpur katika jimbo la Jharkhand, mashariki mwa India.
Alifanya vyema chuoni lakini anasema wenzake chuoni wamepata kazi lakini yee hajabahatika.
"Watu huogopa kunipa kazi," anasema Saddam, na kuongeza kwamba huenda kampuni zinaogopa kwamba atatatizika kusafiri nje ya nchi hiyo.
Alifikiria huenda angetatua tatizo hilo kwa kupata pasipoti mpya, leseni ya udereva na nyaraka nyingine akitumia jina lake mpya la Sajid.
Lakini sasa vyeti vyake havilingani majina.
Ana kikao na mahakama 5 Mei kutaka kuwashurutisha maafisa wa elimu kubadilisha jila la vyeti vyake vya shule.

Watu 20 wafariki dunia baada ya kuangukiwa na mti mkubwa

Watu takriban 20 wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mti mkubwa kuwaangukia wakiogelea katika maporomoko ya maji eneo la Kintampo, Ghana.
Maporomoko hayo ni maarufu sana kwa watalii.
Watu hao walikuwa wakiogelea pale upepo mkubwa ulipoangusha mti na kusababisha mkasa huo, maafisa wa huduma za dharura wamesema.
Msemaji wa taifa wa huduma za dharura Prince Billy Anaglate alisema kisa hicho kilitokea katika maporomoko ya Kintampo, katika jimbo la Brong-Ahafo.
Kikosi cha pamoja na polisi na wahudumu za dharura kilifika eneo la mkasa kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo.
"Mti mkubwa ulianguka mvua kubwa iliyoandamana na upepo ilipokuwa inanyesha na kuwaangukia watu hao," aliyeshuhudia aliambia Starr News ya Ghana.
"WEngi walikuwa wanafunzi wa shule ya upili ya Wenchi Senior High. Wengine ni watalii.
Tunajaribu kuwaokoa waliokwama chini ya mti huo kwa kuukata mti huo na matawi yake kwa msumeno."
Bw Anaglate aliambia AFP kwamba wanafunzi 18 walifariki papo hapo na wengine wawili wakafariki wakitibiwa hospitalini.
ALisema watu 11 kwa sasa wanapokea matibabu, akiwemo mmoja wa maafisa wa shule hiyo aliyekuwa anasimamia ziara hiyo ya wanafunzi.
Taarifa nyingine zinasema waliojeruhiwa ni zaidi ya 20.
Wanatibiwa katika hospitali ya manispaa ya Kintampo.
"Tunatuma salamu za rambirambi kwa familia za waliofariki na kuwaombea waliojeruhiwa," waziri wa utalii wa Ghana Catherine Abelema Afeku alisema kupitia taarifa.

Utashangaa zaidi, Gharama ya kuilinda familia ya Trump kwa siku moja

Familia ya Rais wa Marekani, Donald Trump ina ulinzi mkali. Ulinzi huo unadaiwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
Wakati ambapo Trump alihamia kwenye ikulu ya White House iliyopo jijini Washington DC, mke wake Melanie, na mwanae wa mwisho, Barron bado wanaishi New York.
Muda mfupi baada ya uchaguzi, ripoti ya CNN Money ilionesha kuwa kuilinda familia ya Trump mjini New York hugharimu dola milioni 1 kwa siku.
Kama wakiamua kuungana na Trump White House, gharama hiyo itapungua kwa kiasi kikubwa.
Hilo si jambo pekee linalozungumzwa kwa sasa. Tangu mwaka uanze, Trump ameenda mapumzikoni mara nne huko Mar-a-Lago Florida. Kwa mujibu wa wachambuzi wa gazeti la Politico, safari hiyo hugharimu dola milioni 3 kila akienda.

Sunday, March 19, 2017

Korea Kaskazini 'yafanyia majaribio injini mpya ya kurusha roketi'

Vyombo vya habari nchini Korea Kaskazini, vinasema kuwa taifa hilo limefanyia majaribio injini moja kubwa maalum yenye uwezo wa kurusha angani mtambo wa Satellite.
Kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong Un, amenukuliwa akisema kuwa, injini hiyo mpya itaisaidia Korea Kaskazini, kufikia uwezo wa kimataifa wa kufyatuaji Satellite angani.
Wachanganuzi wanasema majaribio ya mtambo huo wa kurusha angani roketi--ambayo bado haijathibitishwa-- pia itakuwa jambo la kuangaliwa kwa undani katika nia ya Pyongyang kuunda zana za kinuklia zenye masafa marefu.
Tangazo hilo linatokea wakati wa waziri wa maswala ya nchi za kigeni wa Marekani, Rex Tillerson, anapofanya mazungumzo na viongozi wa China huko, Beijing.
Awali, Bwana Tillerson, aliionya Marekani kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini, kwamba inaweza kuharibu mambo hata zaidi.

Schulz apitishwa kuwania ukansela dhidi ya Merkel

Martin Shulz Jumapili (19.03.2017) amechaguliwa rasmi kugombea Ukansela dhidi ya Angela Merkel katika uchaguzi uliopangwa kufanyika hapo mwezi wa Septemba kumn'gowa mwanamke ambaye anatajwa kuwa shupavu kabisa duniani.
Mwanasiasa huyo wa chama cha Social Demokrat ambaye tayari anasifiwa kwa kukipa nguvu upya chama chake amechaguliwa kwa kauli moja kuwa kiongozi wa chama cha SPD na mgombea katika mkutano wa chama wa siku moja uliofanyika mjini Berlin.
Hotuba yake kwa viongozi na wanachama wa chama hicho Schulz mwenye umri wa miaka 61 amejaribu kuimarisha kasi ya umashuhuri wake dhidi ya Merkel ambaye muungano wake wa kihafidhina miezi michache iliopita ulikuwa ukiongoza kusikopingika.
Ameuambia mkutano huo wa chama chake "kuanzia sasa mapambano ya kuwa chama kikuu yanaanza nchini kuuchukuwa Ukansela."
Uamuzi wa Shulz kuondoka bunge la Ulaya ambapo amekuwa akiliongoza kwa miaka mitano kama spika na kuwa ngonbea uongozi wa Ujerumani umekipa chama cha SPD pumzi mpya tokea mkuu wa zamani wa chama hicho Sigmar Gabriel alipomtaka ashike hatamu za kukiongoza hapo mwezi wa Januari.
Shulz ameiambia radio ya umma ya Berlin RBB wiki hii "inatia moyo kuona kwamba katika wiki chache zilizopita watu wameanza kuwa na matumaini kwamba chama cha SPD kimepata nguvu kutaka ushindi wa uchaguzi.
Amesema ni dhahir kwamba nia yake ya kutaka kutekeleza sera ambazo zitaboresha kidogo hali ya maisha ya wachapa kazi imefanya watu wengi wamuunge mkono.
Uchunguzi wa maoni umeonyesha chama cha SPD kimejipatia pointi kumi katika wiki za hivi karibuni wengine wakikiweka mbele ya muungano wa kihafidhina wa Merkel ambaye anataraji kushinda muhula wa nne madarakani.
Chama cha SPD kimefytuwa risasi ya kwanza ya kuanza kampeni ya uchaguzi mkuu na pia uchaguzi wa majimbo matatu ya Ujerumani ambao wa kwanza utafanyika Saarland kwenye mpaka na Ufaransa hapo Machi 26.
Ameliambia gazeti la Bild Jumapili kwamba wote wawili yeye na Angela Merkel wana sifa za kuwa kansela.
SPD yachoshwa na serikali ya mseto
Chama cha Social Demokrat washirika wadogo katika serikali ya mseto ya Merkel kwa takriban miaka minane kati ya kumi na mbili iliopita imekuwa chini ya kuvuli cha Merkel.Lakini Gabriel ambaye sasa ni waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani amewaambia wafuasi mwezi huu kwamba kuingia kwa Shulz katika kinyan'ganyiro hicho cha Ukansela akiwa mtu nje ya serikali kumewavutia wapiga kura wengi wa chama cha SPD ambao wamechoka kuwamo katika serikali ya mseto ya ya"muungano mkuu".
Historia ya Schulz ni ya aina yake alitaka kuwa mchezaji wakabumbu wa kulipwa,hakumaliza shule ya sekondari aliweza kuachana na tabia ya ulevi wa kupindukia na alifunguwa duka la vitabu na kujifunza lugha tano.
Wanachama wa chama chake wanatumai Shulz ataweza kuondowa mgawanyiko uliko kwenye chama hicho kutokana na mpango wa mageuzi ya soko la ajira unaojulikana kama Agenda 2010 uliopitishwa na kansela wa mwisho wa chama cha SPD Gerhard Schroeder ambaye alishindwa na Merkel hapo mwaka 2005.

Friday, March 17, 2017

Meli ya mizigo ya Uturuki yazama Libya

Meli moja ya mizigo ya Uturuki imeripotiwa kuzama na wafanyakazi 7 wa meli hiyo hawajulikani walipo.
Msemaji wa jeshi la majini wa Libya Ayoub Qassem alifahamisha kuwa wafanyakazi 6 wa meli hiyo waliweza kuokolewa baada ya kuomba msaada walipokuwa kilomita kadhaa kutoka bandari ya Misrata .
Jenerali Qassem aliendelea kusema kuwa shughuli ya kuwatafuta waliopotea inaendelea ingawaje bahari imehafuka na mawimbi makali.
Meli hiyo aina ya Tınaztepe S ilikuwa imebeba marumaru na kwa baharti mbaya ikazama kwa ajili ya hali mbaya ya hewa .
Libya ni nchi ya tatu inayoongoza barani Afrika baada ya Misri na Algeria kwa kununua bidhaa zake kutoka Uturuki.

Mali yafungiwa na FIFA michuano ya kimataifa

Fifa imetangaza kuifungia nchi ya Mali kushiriki michuano ya kimataifa kwa madai ya serikali kuingilia masuala ya soka.
Waziri wa Michezo wa Mali, Housseini Amion Guindo aliamua kuunda kamati ya muda kuendesha Shirikisho la Soka la Mali (Femafoot) baada ya kuona uongozi uliokuwa madarakani kutokuwa sahihi.
Lakini baada ya Femafoot kufikisha malalamiko yake Fifa, shirikisho hilo la soka la limataifa, likaiamuru serikali ya Mali, kuvunja kamati hiyo hadi Ijumaa.

Leseni ya mtoto kutoka kwa wazazi 3 yatolewa Uingereza

Madaktari mjini Newcastle nchini Uingereza wamepewa leseni ya kwanza nchini Uingereza kutengeza watoto kutoka kwa wanawake wawili na mwanamume mmoja, shirika la kuthibiti rutba limesema.
Mfumo huo mpya wa aina ya IVF utatumika kuwalinda watoto kutofariki kutokana na magonjwa yanayosambazwa kupitia jeni.
Kundi hilo katika kituo cha rutba za uzazi cha Newcastle kimesema kuwa ni habari njema kwa wagonjwa.
Na sasa kituo hicho sasa kinatarajia mtoto wa kwanza kuzaliwa 2018 ikiwa ndio mapema.
Mfumo huo unalenga kukabiliana na magonjwa ya jeni ambayo huwawacha watu kukosa nguvu za moyo wao kufanya kazi.
Baadhi ya watu wamepoteza watoto kadhaa kwa sababu ya ugonjwa huo.
Ugonjwa huo husambazwa kutoka kwa mama, kwa hivyo mbinu ya kutumia yai lililofadhiliwa, na yai la mama pamoja na mbegu za kiume za baba imeimarishwa.
Mtoto anayepatikana huwa na vinasaba vya jeni kutoka kwa mfadhili, lakini mfumo huo sasa ni wa haki na sasa unafuata maadili na uko tayari kufanyakazi kisayansi.

Kenya kujenga kituo cha umeme cha nyuklia kabla ya mwaka 2027

Kenya imesema inapanga kujenga kituo cha kwanza cha kuzalisha umeme kwa nishati ya nyuklia kabla ya mwaka wa 2027. Waziri wa nishati na mafuta wa nchi hiyo Bw. Charles Keter amesema kabla ya kutimiza ndoto hiyo, Kenya inatakiwa kufikia vigezo vikali vilivyowekwa na Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA. Kwa mujibu wa waziri huyo, Kenya inapanga kutumia dola za kimarekani bilioni 5 kujenga kituo hicho, ambacho kinatarajiwa kuongeza maradufu uwezo wa kuzalisha umeme nchini humo.

Msemaji Wa Jeshi La Polisi Uganda Kwa Kupigwa Risasi

KAMPALA: Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana. Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.

Msemaji Wa Jeshi La Polisi Uganda Kwa Kupigwa Risasi

KAMPALA: Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Felix Kaweesi amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana. Taarifa zinasema Bw Kaweesi ameuawa baada ya gari lake kumiminiwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa anaondoka kwake nyumbani Kulambiro, Kisaasi kaskazini mashariki mwa mji mkuu Kampala.
Walinzi wake wawili walioandamana naye pia wameuawa.
Bw Kaweesi aliteuliwa kuwa msemaji wa polisi Agosti mwaka jana.
Taarifa zinasema alikuwa njiani kwenda kuwahutubia wanafunzi katika chuo kikuu cha Uganda Christian University alipokumbana na mauti yake. Wanafunzi walikuwa tayari wamekusanyika ukumbini katika chuo hicho.
Miili ya watatu hao imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Mulago.

Watu 40 waliuawa katika shambulizi la msikiti Syria

Mpaka sasa hakuna aliyetaja kufanya shambulizi hilo
Wanaharakati wanasema kuwa takriban watu 40 waliuawa wakati msikiti mmoja Kaskazini Mgharibi mwa Syria ulipolipuliwa na ndege za kivita ambazo hazikufahamika.
Muangalizi mmoja wa haki za binaadam nchini Syria anayetokea nchini Uingereza amesema msikiti huo ulishambuliwa wakati watu wakiwa kwenye swala ya alasiri.
Kundi moja la wafuatiliaji wa mambo linasema msikiti huo ulikuwa katika eneo ambalo linashikiliwa na waasi.
Jeshi la Marekani linasema siku ya Ahamis liliwaua baadhi ya wapiganaji wa Al Qaeda kwa kutumia ndege za kivita wakati wakiwa kwenye kikao chao eneo moja liitwalo Idlib.
Taarifa hiyo haijataja kuwepo kwa vifo ama kujeruhiwa kwa wananchi wa kawaida.