Meli moja ya mizigo ya Uturuki imeripotiwa kuzama na wafanyakazi 7 wa meli hiyo hawajulikani walipo.
Msemaji wa jeshi la majini wa Libya Ayoub Qassem alifahamisha kuwa wafanyakazi 6 wa meli hiyo waliweza kuokolewa baada ya kuomba msaada walipokuwa kilomita kadhaa kutoka bandari ya Misrata .
Jenerali Qassem aliendelea kusema kuwa shughuli ya kuwatafuta waliopotea inaendelea ingawaje bahari imehafuka na mawimbi makali.
Meli hiyo aina ya Tınaztepe S ilikuwa imebeba marumaru na kwa baharti mbaya ikazama kwa ajili ya hali mbaya ya hewa .
Libya ni nchi ya tatu inayoongoza barani Afrika baada ya Misri na Algeria kwa kununua bidhaa zake kutoka Uturuki.
0 comments:
Post a Comment