Wednesday, April 26, 2017
Ray Kigosi afunguka juu ya Diamond na Kanumba kudaiwa kuwa Freemason
Saturday, March 25, 2017
Barakah The Prince ajikita kwenye kilimo cha mboga mboga
Harmonize atimka baada ya kukutana na meneja wa Harmorapa kwenye kipindi
Friday, March 17, 2017
Baba : Dna ya Mtoto wa Diamond lazima.
WAKATI Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kujaaliwa kupata mtoto wa pili ambaye ni Nillan, baba mzazi wa msanii huyo, Juma Abdul amesema kuna ulazima wa mjukuu wake huyo kupima DNA ili kuzima zile tetesi kuwa, si wake.
Rais Magufuli alimpongeza Diamond Jumanne wiki hii baada ya kiongozi huyo wa nchi kupiga simu kwenye Kipindi cha 360 cha Clouds TV wakati Diamond akihojiwa ambapo alisema: “Hongera sana Diamond kwa kumpata mtoto mwingine, wakati wa kampeni ulikuwa na mtoto mmoja, sasa umeongeza wa pili, nakupongeza sana.”
ISHU YA DNA SASA
Awali, baada ya Zarinah Hassan ‘Zari’ kujifungua mtoto huyo nchini Afrika Kusini, yaliibuka madai mtandaoni kuwa, mtoto huyo anafanana sana na aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga na kwamba kuna uwezekano uchepukaji ulichukua nafasi yake. Madai hayo yaliyofanana na yale ya kipindi kile Diamond alipompata Tiffah, yalishika kasi na kufikia wakati baadhi wakawa wanaunganisha picha ya Nillan na Ivan kisha kuonesha jinsi sehemu nyingi za usoni zilivyofanana.
Licha ya maneno hayo kuenea kila kona na wengine kutaka kuamini kuwa huenda kuna ukweli, Diamond amekuwa mkimya licha ya wakati f’lani kuwahi kusema kuwa, hana sababu ya kujibizana na watu wasiojua ukweli kwani yeye anaamini watoto waliozaliwa na Zari ni damu yake.
“Unajua mwanamke akiwa na mimba hupaswi kusema ana mimba yangu maana huna uhakika, lazima uwe na wasiwasi maana ndiyo akili, akishajifungua kama hivi ndiyo unasema ni mtoto wako maana nikimwangalia anafanana kila kitu na Tiffah na ni kopi yangu kabisa,” aliwahi kusema Diamond.
BABA WA DIAMOND ATIA NENO
Katika kutaka kupata maoni ya baba wa Diamond, Mzee Abdul Juma juu ya haya madai kuwa mjukuu wake, Nillan anafanana na Ivan alisema kuwa, katika hali ya kawaida ili kuwazima wale wenye dhana potofu kwamba mtoto si wa Diamond ni lazima vipimo vya DNA vifanyike.
“Mimi kama mzazi namshauri Diamond akapime DNA ili apate uhakika zaidi japokuwa tunaamini hao wajukuu wetu ni watoto wake lakini kwa kuwa maneno yamekuwa mengi kila kukicha ni lazima afanye hivyo, naamini na maneno ya watu kumsimanga yataisha,” alisema Mzee Abdul na kuongeza:
“Katika maisha ya kawaida kwa mwanaume ni aibu kulea watoto ambao unajua kabisa si wako lakini unasema ni wako. Mpaka Diamond anaamini ni watoto wake na sisi ndugu tunaamini hivyo, kwa nini wengine wasikubaliane na ukweli huo.”
DIAMOND AFANYA YA MAKONDA
Kuhusiana na hili la DNA, watu wamelifananisha na lile na Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kudaiwa kuwa ana vyeti feki na kuona ni kelele za watu wasiomtakia mema, hivyo kuuchuna. Anachokifanya Diamond ni hichohicho, kukausha akijua ipo siku watu watanyamaza
Kajala Masanja: Sijashindwa kumlea mwanangu
Muigizaji wa Filamu Tanzania Kajala Masanja amewafungukia wanaomsema kwamba ameshindwa kumlea binti yake ' Paula' na kusema anatamani awaoneshe watu hao malezi anayompatia binti yake huyo.
Akipiga story na eNewz, Kajala amedai kuwa hawezi kushindwa kumlea mtoto wake na kwamba malezi anayompatia binti yake ni tofauti na yale watu wanayoyazungumzia katika mitandao ya kijamii na kuongeza kuwa binti huyo analelewa katika maadili, yanayotakiwa.
"Sijashindwa kumlea mtoto wangu, natamani wangekuwa wanaona malezi ninayompatia Paula kwani kila wanachokiona na kukisikia kwenye mitandao ni tofauti sana na ninavyomlea". Kajala alisema.
Kajala ameongeza kwamba katika jambo linalomuumiza ni watu kutumia jina la binti yake hyo na kujifanya ni yeye na wakati mwingine kuweka vitu hasi ambavyo vinamfanya mtoto wake achukuliwe tofauti katika jamii.
Aidha muigizaji huyo ameongeza kuwa serikali inapaswa kushughulikia matatizo yanayotolewa na watumiaji wa mitandao kwa umakini wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuweka nguvu ya kutosha.
“Ile akaunti siyo ya Paula kwanza, kwani hajawai kuwa na simu au kumiliki, nimeshawahi kuwaambia wamiliki wa ukurasa huo wabadilishe jina au waandike ni ‘fanpage’ lakini naona wamegoma , Baba yake naye amejaribu kuzifunga lakini bado zinaendelea kutumika mpaka sasa nimechoka ila bado hatujajua tuchukue hatua gani". Kajala aliongeza.
Paula ambaye ni mtoto wa muigizaji huyo pamoja na Producer P- Funky Majani aliwahi kukutwa na mkasa wa kufananishwa na binti aliyerekodiwa akiwa mtupu na kusambazwa mitandaoni.
Gabo awafungukia 'ma-director' wasio na uwezo
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Gabo Zigamba amewataka waongozaji filamu Tanzania (Directors) kutojihusisha na kazi za kuongoza filamu kama hawana vipaji pamoja na taaluma hiyo.
Gabo amesema watu hao ndiyo wanasababisha soko la filamu nchini kupigwa bao na kazi kutoka nje kwa maana kazi wanazozitengeneza kukosa ubunifu na ushindani kama ilivyokuwa zamani kupelekea watazamaji kuichukia 'Bongo Movie'.
"Kuwa 'director' siyo suala la kukurupuka tu, si maamuzi ya kufikirika tu ukaamua kufanya hivyo lakini kila kinachofanyika lazima kiwe kina taaluma ila nasisitiza na kuwaambia watu wasifanye vitu bila ya kuwa na taaluma navyo, ukifanya kitu chenye taaluma nacho itakuwa kwenye ubora".Alisema Gabo
Aidha msanii huyo amesema kwa upande wake watu wasahau kwa sasa kwa yeye kuwa muongozaji filamu na kama atataka kufanya hivyo basi atafanya kwa utaalamu na siyo kukurupuka.
Lulu Atoa Povu Uchumba Wake Kuvunjika
JUZIKATI yaliibuka madai kwamba, uchumba wa staa wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na yule bosi wa redio Bongo umevunjika huku kila moja akiongea lake. Madai hayo yalienea kwenye mitandao ya kijamii na wapo waliokwenda mbali zaidi kudai kuwa, sasa Lulu karejea kwao na ana mpango wa kuanzisha maisha yake mengine.
“Wamemwagana, uchumba haupo tena, ila kusema ukweli inauma kuachwa na umpendaye,” aliandika mdau mmoja kwenye Mtandao wa Instagram kisha akasindikiza maneno hayo kwa picha ya Lulu na baby wake huyo.
Kufuatia madai hayo kusambaa mithili ya moto wa kifuu huku mashabiki wengi wa mastaa hao wakipiga simu kwenye chumba chetu cha habari na kutaka ufafanuzi wa habari hizo, Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Lulu kupitia simu yake lakini alipoulizwa, badala ya kutoa ufafanuzi alitoa povu kuashiria kuwa hataki habari zake ziandikwe.
“Sitaki kuongelea chochote…sitaki kuongelea chochote, pliz…unajua mimi siyo mtu wa magazeti kabisa na unanijua vizuri…” alisema Lulu na kumuacha mwandishi ameduwaa hasa kwa ile sentensi kwamba eti yeye si mtu wa magazeti.
Diamond: Mwandishi ukiniandika kwa ubaya unapoteza muda wako
CEO wa Wasafi, Diamond Platnumz amedai kuwa kitendo cha baadhi ya watangazaji na waandishi kushikilia kumzungumzia na kumuandika kwa Mambo mabaya, cha kujipotezea muda kwao.
Kwenye exclusive interview na Prince Ramalove kupitia Kings FM, Diamond Alifafanua kauli yake ya kusema kuwa yeye hategemei Redio wala TV pindi anapotoa nyimbo zake kwa sasa.
“Unajua kwamba kuna kiwango unapofikia,unapokuwa na mashabiki wengi,lazima uongeze ufanisi wako wa usambazaji wa kazi zako.Tuna redio tuna TV, lakini pia lazima tuongeze namna zingine za kupromote kazi zako,” amesema Diamond.
“Wasanii wanatakiwa wajiongeze, sasa naona kuna watu wameichukua tofauti na kuipindua kumtengenezea mtu baya,lakini wanapoteza muda.”
Diamond ameongeza kuwa yeye anaheshimu vyombo vya habari na hata kama kuna watu wanadai amefika alipo kwa mchango wao, yeye anaheshimu pia.
Wednesday, March 15, 2017
Nuh Mziwanda Apata Mtoto Wa Kike
Nuh Mziwanda na mkewe Nawal wamefanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza wakike.
Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muimbaji huyo amesema kuwa mke wake amejifungua jana usiku na tayari wamempatia jina la Anyagile.
Nuh na Nawal walifanikiwa kufunga ndoa mwezi Novemba mwaka jana. Wakati huo huo hitmaker huyo wa Jike Shupa ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Anameremeta’.
‘Dogo’ Harmorapa ainunua bifu ya Diamond na Alikiba, achezea mvua ya matusi
Harmorapa ni kama amemwaga petrol kwenye moto wa gesi. Rapper huyo aliyeteka vichwa vya habari kwa sasa nchini ameonekana kuanza kuununua ugomvi wa Diamond na Alikiba.
Harmo kupitia mtandao wa Instagram, amemtuhumu Diamond kuwa ndio aliyeanza kumchokoza Kiba hivyo anapaswa kumuomba msamaha kupitia vyombo vya habari. Kupitia mtandao huo hitmaker huyo wa Kiboko ya Mabishoo ameandika:
Mimi harmorapa mfalme wa bongoflaver and social network kwa sasa nasema kiukweli kutoka moyoni bwana mdogo #diamondplatnumz wewe ndo ulie anza kumrushia vijembe vya dharau Fundi #alikiba sasa usitafute suluhu kirahisi rahisi wewe platnumz nenda kwenye midia piga goti Muombe msamaa #alikiba kwani mkosefu ni wewe na sio #alikiba .
#now_naitwa_harmo_simba
Matokeo ya alichokiandika si mazuri. Hadi tunaenda mtamboni, bado anachezea mvua ya matusi kutoka kwa Team Diamond.
Dayna: Simchukii Baba watoto wangu
Dayna Nyange
NYOTA wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amesema licha ya mambo mengi kutokea katika uhusiano wake na mwanaume aliyezaa naye mtoto wa kike, hawezi kumchukia hata mara moja.
Akichonga na Risasi Vibes, Dayna alikiri kutokuwa na mawasiliano kabisa na baba mtoto wake huyo anayedaiwa kuwa yupo Afrika Kusini, lakini ikitokea wakakutana na kumtaka mwanaye, hatasita kumpa kwa sababu ni mtu ambaye tayari wameshaunganisha damu na kutengeneza undugu.
“Unajua ni kweli kuwa katika uhusiano wangu nilipitia mambo mengi ya kuumiza yaliyosababisha mpaka tukaachana, lakini hayawezi kusababisha nikamchukia mzazi mwenzangu huyo maana tayari sisi ni ndugu,” alimaliza Dayna
Monday, March 13, 2017
Rose Muhando Asakwa Apelekwe Soba
DAR ES SALAAM: Taarifa mbaya ya kusikitisha kutoka kwa staa wa nyimbo za Injili, Rose Muhando zinadai kuwa, mwimbaji huyo anasakwa na uongozi wa Sober House ya Pederef ili waweze kumwokoa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya ‘unga’.
Chanzo kilicho karibu na mwanamama huyo ambaye amejijengea jina kubwa kupitia nyimbo zake nzuri kama Nibebe, kimeeleza kuwa Rose ametoweka nyumbani kwake mjini Dodoma baada ya kutopea kwenye matumizi ambapo kuna kiongozi mmoja wa dini ameamua kumsaidia.
“Kuna kiongozi mmoja wa dini hapa Dodoma, ameamua kujitolea kumsaidia Rose baada ya kusikia hali yake ni mbaya. Ameamua kuwatafuta Pederef ili wamsake popote alipo na wakimpata wampeleke soba moja kwa moja na gharama zote yeye atazishughulikia,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, mwanahabari wetu alimvutia waya Rose ili kuzungumzia madai hayo ambapo alipopatikana alioomba aachwe kwani alikuwa kanisani, angempigia mwandishi baadaye.
“Nitakupigia baadaye, nipo kanisani…,” alisikika Rose na kukata simu. Hata alipopigiwa tena baadaye, simu yake haikupokelewa.
Hata hivyo, Wikienda ilimtafuta mmliki wa Sober ya Pederef, Nuru Saleh aliyekiri kupewa kazi ya kumtafuta Rose na kumfikisha katika soba yao iliyopo Dodoma na kuanza kumpatia tiba ya kuacha matumizi ya madawa ya kulevya.
“Ni kweli. Sisi ndiyo kazi yetu. Nimepewa hiyo kazi na kiongozi wa dini, naomba nisimtaje lakini tumeshaanza kumtafuta na tukimpata tu, tutampeleka kwenye soba yetu ya Dodoma,” alisema Nuru.
Mara kadhaa Rose amewahi kuripotiwa kuwa anabwia unga lakini mwenyewe amekuwa akikanusha.
Wema Sepetu Ajadiliwa Msikitini Dar
DAR ES SALAAM: Makubwa! Wema Isaac Sepetu amezua gumzo baada ya kujadiliwa kwenye msikiti mmoja uliopo Mwenge jijini Dar kufuatia mhadhiri mmoja maarufu aliyefahamika kwa jina moja la Mwaipopo kuelezea namna mwanadada huyo alivyotoa mchango wake kumsaidia marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ alipokuwa mgonjwa.
Akizungumza kwenye msikiti huo akiwataka Waislam wamchangie fedha kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, mhadhiri huyo alisema kuwa anawashangaa Waislam kutokuwa na mioyo ya kuwasaidia wenzao wanapokuwa na matatizo wakati dini haitaki hivyo.
“Nimezunguka sana kwenye misikiti mingi lakini msaada ambao nimekuwa nikipata kutoka kwa Waislam wenzagu haukuwa wa kuridhisha, inasikitisha sana.
Kuna wakati yule msanii wa filamu, Sajuki alipokuwa anaumwa, akina Wema walimchangia mapesa na akaenda kutibiwa lakini sisi tumekuwa wagumu katika kutoa,” alisema mhadhiri huyo.
Baada ya kusema, hivyo baadhi ya watu waliokuwa msikitini hapo walianza kunong’ona chinichini wakimjadili Wema huku wengi wakisema kuwa inakuwaje staa huyo awe na moyo wa kutoa kushinda waumini wa Kiislam wengine ambao wamejaliwa utajiri. “Wewe fikiria kama Wema ameweza kutoa pesa zake nyingi tu kusaidia katika matibabu ya Sajuki kipindi kile, Waislam kwa nini tunakuwa wagumu,” alihoji kijana mmoja aliyekuwa msikitini hapo.
Hata hivyo, hoja ya mhadhiri huyo ambaye historia yake inaonesha alikuwa Mkristo ni kwamba, Waislam wanatakiwa kusaidiana katika shida na raha pamoja na kwamba alikosolewa kuwa aliyemsaidia Sajuki fedha nyingi kipindi kile hakuwa Wema bali alikuwa ni Jacqueline Wolper.
Harmorapa amchana Mose Iyobo
Baada ya kuachia track mpya iliyojaa utata utata hivi, Harmorapa ameweka kila kitu ‘clear’ kilichomfanya kuandika mistari ya kumdiss dancer wa Diamond, Mose Iyobo.
Kupitia kipindi cha Fleva Plus kinachoruka hewani kupitia Sunrise Radio, DJ Dix alimuuliza kuhusu chanzo cha kile kinachoendelea kati yake na dancer huyo kutoka WCB.
Harmorapa hakuona noma na alijibu maswali yote aliyoulizwa. Sauti yake iliskika ikisema kwamba Mose Iyobo aambiwe kwamba anahitaji dancer na angetaka awe ni yeye. Aliongeza kuwa anatumia dollars kwahiyo ana uwezo wa kumuajiri na kumlipa vizuri tu.
“Mwambie Mose Iyobo nahitaji dancer, yeah nahitaji dancer kwa sababu naweza mimi, nahitaji dancer so naweza kumlipa kwa sababu Harmorapa ana dollar na pia anatumia account ya dollar,” alisema.
Katika hatua nyingine, alipoulizwa ni kwa nini aliamua kumdiss jamaa kwenye ngoma yake aliyomshirikisha Juma Nature ‘Kiboko Ya Mabishoo’, alisema…”Yani hata mfano naianza ile ngoma nilivyoiandika na nini, mwanzo haikuwa vile ila baada ya kuja kunianza mimi ndo pale nikapata feelings sana nikajikuta naandika vitu ambavyo vinamdiss pia na yeye ili nimjibu.”
Harmorapa anahisi Mose Iyobo alichokoza nyuki pale alipomfananisha na nyani kwa hiyo kung’atwa ni kitu cha lazima. Katika hatua nyingine, rapper huyo alipinga kinachoonekana kama ana nguvu nyingi kwa upande wa ‘publicity stunt’ kuliko muziki wake.
Hali kadhalika, amewataka mashabiki zake wawe tayari kupokea kazi zake kwa kuwa amejipanga vizuri kimuziki mwaka huu.
Sunday, March 12, 2017
Instagram: Post ya Idriss Sultani Kuhusu Jokate Mwegelo
Zilizojitokeza Leo March 12 2017 kwenye mitandao ya kijamii ni pamoja na post za mastaa na moja ya post nilizopenda zisikupite ni hii ya Idriss Sulutani ambapo amempongeza Jokate Mwegelo kutokana na mchango mkubwa katika jamii baada ya kutumia Brand yake kuitumikia jamiii na kubadilisha maisha ya vijana wengi.
Idriss ameyaandika haya kwenye Post hiyo…>>>Ndani ya miaka 5 she has done so much more than any celebrity in Tanzania kwenye jamii. Naomba nihamishie upepo kwake kwa shukrani zote kwa yote aliyoyafanya kuinyanyua jamii ya watanzania na naomba msamaha kwa niaba ya watanzania kwani tulikua busy tunaangalia nani anatoka na nani na nani kagombana na nani na nani kaposti uchi leo,
tukasahau kua umebadilisha maisha ya vijana zaidi ya laki 5 ndani ya miaka miwili tu. Ingekua muamuzi ni mimi ungekua Forbes because ni celebrity pekee uliyesimamisha brand product yako kwa jina lako and yes African boy ya Jux inakuja pia. Uliyoyafanya kwenye jamii yako bila kulazimishwa ni zaidi ya baadhi viongozi tuliowachagua kufanya kazi hizo tunazowalipa kufanya.
If am allowed may I please say you are “THE FLOWER OF TANZANIA” if you ask me why its because you are beautiful and you make us smell good werevaa you go.
Kwa niaba ya watanzania ningependa kusema tumejisahau sana na tusamehewe. Stay beautiful .. cc:
@jokatemwegelo#TheFlowerOfTanzania
Sakata la Ben Saanane lachukua sura mpya
Dar es Salaam. Sakata la kupotea kwa mkuu wa Idara ya Sera na Utafiti wa Chadema, Ben Saanane limechukua sura nyingine baada ya Umoja wa Mataifa (UN) kusema upo tayari kutuma watu nchini kwa ajili ya uchunguzi.
Saanane, ambaye pia ni msaidizi wa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alipotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 18 mwaka jana na hadi sasa haijaeleweka kuwa alitekwa au kuuawa, ingawa Chadema imehusisha kutoweka kwake na taarifa ambayo Saanane aliitoa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utata wa elimu ya baadhi ya viongozi.
Siku chache baada ya kupotea kwa Saanane, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliitaka Serikali kueleza kama inamshikilia kada huyo au ifanye uchunguzi wa kina kuhusu kupotea kwake.
Sanjari na hilo, Lissu aliitaka Serikali kufuatilia ujumbe wa vitisho ambao Saanane aliwahi kutumiwa kwenye simu yake ya mkononi na mtu ambaye bado hajafahamika.
Akisisitiza msimamo wa chama chake, Lissu alizitaka mamlaka zote husika na usalama wa raia ziseme hali halisi inayozingira sintofahamu ya mahali alipo, ikiwa yuko ndani ya nchi au nje, au hata kama amefariki na kuzikwa kwa kutotambuliwa.
Wakati utata huo ukiendelea, ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu duniani ya UN yenye makao yake makuu jijini Geneva, Uswisi, imesema iko tayari kutuma timu wa uchunguzi.
Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano uliotishwa na ofisi hiyo, Kanda ya Afrika uliohusisha nchi za Sudan, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Ethiopia, Djibouti na Tanzania.
Akizungumza na gazeti hili jana, mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo- Bisimba alisema suala hilo liliibuka baada ya wajumbe wa mkutano huo kutaka kujua undani wa sakata hilo, lakini hakukuwa na taarifa za kina.
“Wajumbe walionyesha kuguswa na suala la mtu kupotea katika mazingira ya utata na kutaka tuelezee kwa undani ilivyokuwa. Hatukuwa na taarifa za kina hivyo wakasema wako tayari kulifanyia kazi endapo tutatuma urgent alert,” taarifa ya dharura.
“Taarifa tutakayotuma ndiyo itakayowawezesha wao kutuma timu ya uchunguzi ije hapa baada ya hapo watajua ni kitu gani waseme kwa Serikali.”
Dk Bisimba alieleza kuwa bado taarifa hiyo haijaandikwa kutokana na kuwasubiri ndugu wa Saanane ambao wanatakiwa kutoa maelezo kwa kina.
“Tuliwaambia ndugu zake waje tupate maelezo yatakayotuwezesha kuandika hiyo urgent alert, lakini bado hawajaja. Watakapofika tutaandika na kuituma ili uchunguzi ufanyike.”
Alipotafutwa kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa suala hilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai(DCI), Kamishna Robert Boaz alisema: “Nitafute Jumatatu kwa sasa nipo kwenye kikao.”
Friday, March 10, 2017
Aika (Navy Kenzo) afunguka haya kuhusu Vanessa Mdee
Muimbaji wa kundi la Navy Kenzo, Aika, amedai kuwa Vanessa Mdee ndiye aliyewahamasisha kurudi kwenye muziki baada ya kuwa wamekata tamaa.
Akizungumza jana kwenye kipindi cha Ngaz Kwa Ngaz cha EATV ambapo yeye na Nahreel walikuwa ma-hosts, Aika amemuelezea Vee Money kama mtu mwenye upendo.
“Ni msichana ambaye ana bidii, ametumotivate vitu vingi sana hata sisi kwenye maisha yetu,” amesema Aika. “Tuseme, yeye ndiye alitufanya sisi turudi kwenye muziki baada ya kuja studio na kusikiliza nyimbo zetu na kusema ‘jamani toeni hii nyimbo ya Bokodo’ by then. Alitupa nguvu sana na ni mtu ambaye amekuwa akituencourage tukisaidiana,” ameongeza.
Vee Money pia aliwahi kuzungumzia story hii.
Akizungumza kwenye kipindi cha Up Close & Personal cha K24 ya Kenya, Vee alisema alikutana na Nahree na Aika baada ya kupigwa chini na label ya B’Hits.
“Kwahiyo nikasema nahitaji kumpata mtu ambaye anaweza kupatia sauti yangu. Shout out kwa Hermy kwasababu sasa sisi ni familia, ni kaka yangu daima. Kwahiyo nilikuwa naijua hii bendi ya Navy Kenzo toka Arusha na wakati huo walikuwa wakijulikana kama Pah One. Pah One ikaja kuvunjika na wawili kati yao walikuwa wanataka kwenda nje kusoma masters, nilienda kwenye studio yao ambayo wakati huo ilikuwa nyumba yao na nikamuambia Nahreel ‘nakuaminia, nadhani mimi na wewe tunaweza kufanya mambo makubwa pamoja,’” alisema Vanesa.
Saturday, March 4, 2017
Harmorapa amkera Jacqueline Wolper
STAA wa fi lamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameeleza kukerwa na mwanamuziki chipukizi, Athuman Omary ‘Harmorapa’ aliyesema amewahi kutoka naye kimapenzi jambo ambalo siyo kweli.
Harmorapa
Akichonga na Mikito Nusunusu Wolper alisema mwanamuziki huyo ambaye ameimba kwenye wimbo wake wa Kiboko ya Mabishoo kuwa ameshatoka naye kimapenzi amemkosea heshima na hata alivyousikia wimbo huo umemshangaza kwa sababu hata Harmorapa mwenyewe anamuona kwenye mitandao ya kijamii na magazetini tu hajawahi kumuona ‘live’.
“Jamani huku ni kukoseana heshima maana huyo Harmorapa hata simfahamu huwa namuona kwenye mitandao na magazetini tu, sasa alivyoimba ametoka na mimi kimapenzi naona kama ni kituko kikubwa sana,” alisema Wolper.
Wasanii wa filamu wapewa dili na Rose Ndauka
Kampuni ya Ndauka Advert ya malkia wa filamu Rose Ndauka ikishirikiana na African Swahili TV Machi 9,10 itafanya usahili katika ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho kwajili ya kuwapata wasanii ambao watashiriki kwenye tamthilia mpya itwaayo ‘How Cheat?’.
Muigizaji huyo amewataka wasanii wakubwa kwa wadogo kuchangamkia fursa hiyo ili kujipatia ajira pamoja na kukuza vipaji vyao.
“Kipaji chako ndio mtaji wako, kipaji chako ndio ajira yako,” alisema Rose.
Muigizaji huyo ambaye ni mama wa mtoto mmoja amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia filamu.
Jokate afunguka hivi baada ya kuulizwa ‘Nini kinakujia haraka unaposikia jina Rais Magufuli,Makonda, Alikiba, Diamond’
Kila staa ana namna anawaangalia viongozi wa nchi pamoja na wadau kutoka katika nyanja mbalimbali.
Jokate alipata fursa ya kuwazungumzia baadhi ya viongozi pamoja na wasanii na kutoa mtazamo wake jinsi anavyowachukulia.
Mwanamitindo huyo akiwa katika kipindi cha 360 cha Clouds TV Jumamosi hii aliulizwa swali ‘Nini kinakujia kwa haraka unaposikia jina Rais Magufuli, RC Makonda, Zitto Kabwe, Alikiba pamoja na Diamond Platnumz”.
Akijibu swahi hilo Jokate alisema, “Namfahamu Zitto Kabwe kama mtu smart sana, ukitaja jina la Mh Paul Makonda inanijia picha ya “Mbabe wa Vita” . Ukitaja Alikiba inanijia picha ya muimbaji mzuri. Ukitaja Diamond Platnumz namuona mtu mchapakazi (anajituma sana ). Kuhusu Rais Dr John Pombe Magufuli namuelezea kama TingaTinga ( mtu wa kazi ) , Mh Rais yuko vizuri sana,” alisema Jokate.

