Serikali imewaagiza waƙuu wa Mikoa na Wilaya nchini kusimamia na
kuanzisha zoezi la kubaini mipaka ya asili ya maeneo yote na kuyapima
ili kuhakikisha yanapata hati na kwamba zoezi hilo litekelezwe ndani ya
miezi mitatu.
Agizo hilo limetolewa leo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene wakati
akitoa taarifa ya uvamizi wa maeneo ya shule za msingi, seƙondari na
maeneo ya kutolea huduma za afya na masoko yaliyo chini ya ofisi ya Rais
TAMISEMI.
Mhe. Simbachawene amesema ni marufuku kujenga vyumba vya biashara
kuzunguka shule za msingi, sekonɗari na maeneo ya kutolea huduma za
afya, kama chanzo cha mapato kwa sababu kitendo hicho kinasabisha
muingiliano usiokubaliana na huduma zinazopaswa kutolewa kwenye maeneo
hayo.
Amesema maendeleo yoyote yaliyofanywa na yanayotarajiwa kujengwa kwa
ajili ya shughuli hizo hayaruhusiwi, na kwa upande wa shule za msingi na
sekondari zilizopo mijini halmashauri zihakikishe zinajenga uzio
kuzunguka shule hizo ili kudhibiti muingiliano.
Ametoa wito kwa jamii zinazozunguka maeneo hayo kushirikiana na serikali
kwa kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali za mitaa juu ya uvamizi
huo,kwa kuonyesha alama za asili za mipaka ya maeneo hayo kabla ya
kuvamiwa.
Amewataka wananchi waliovamia maeneo hayo ya taasisi hizo waondoke wao
wenyewe vinginevyo hatua za kuwaondoa kwa nguvu zitatumika.
Aidha amesena TAMISEMI kwakushirikiana na wizara ya ardhi wameanza taratibu za kutambua haki miliki za ardhi.
0 comments:
Post a Comment