Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Monday, October 3, 2016

PICHA 8: Rais Magufuli alivyompokea Rais wa Congo, Joseph Kabila leo


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila Kabange, amewasili hapa nchini leo October 03 2016 kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Rais Joseph Kabila Kabange amepokea heshima ya kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake na baadaye kushuhudia burudani ya vikundi vya ngoma.
Hapo kesho October 04 2016 Rais Joseph Kabila Kabange atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli, ataweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na baadaye kushiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
1 2 4 2 67 6 5 8

0 comments:

Post a Comment