Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, October 6, 2016

Viwanja kuwaka moto leo kusaka safari ya Urusi

Leo timu za nchi mbalimbali zitaingia uwanjani kukipiga kusaka tiketi ya kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Miongoni mwa michezo hiyo ni Austria itakipiga dhidi ya Wales, wakati Moldova , ikishuka dhidi ya Serbia, huku, Kosovo ikishuka na Croatia.

Jamhuri ya Ireland watakuwa wenyeji wa Georgia, wakati Albania wakiifuata, Liechtenstein, huku Macedonia wakiwapa mwaliko Waisrael.

Iceland watakuwa nyumbani dhidi ya Finland, huku Waturuki wakiwaalika – Ukraine, na mchezo mkali kabisa hii leo ukiwa kati ya mabingwa wa dunia mwaka 2006 Italia wakimwaga mbungi dhidi ya mabingwa wa dunia 2010 Hispania.

0 comments:

Post a Comment