Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Tuesday, October 4, 2016

PICHA 9: Naibu Waziri Ole Nasha alivyoongoza mazishi ya mmoja ya watafiti waliouawa


Leo October 4, 2016 Naibu waziri wa kilimo mifugo na uvuvi Wiliam Ole Nasha ameongoza wananchi wa Arusha kwenye misa ya kuaga mwili wa marehemu Theresia Alex Nguma katika kanisa la mtakatifu Joseph Mfanyakazi Olasiti jijini Arusha.
Theresia Alex ni mmoja watafiti waliouawa na wananchi wa kijiji cha Ilinga mkoani Dodoma baada ya kudhaniwa ni wanyonya damu. Akizungumza kanisani hapo Waziri Ole Nasha amesema bado serikali inaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Imeelezwa Mpaka kufikia sasa jumla ya watu 45 wamekamatwa na jeshi la polisi mkoani Dodoma baada ya kuhusishwa na tukio kuwauwa kwa mapanga kisha kuwachoma moto watafiti wawili na dereva wa chuo cha  utafiti wa udongo na maendeleo ya ardhi cha Seliani Arusha August 1 mwaka huu.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro pia  ametoa onyo kwa wananchi wenye tabia ya kuchukua sheria mkononi bila badala ya kufikisha kwenye vyombo vya dola.
img-20161004-wa0002
img-20161004-wa0003
img-20161004-wa0004
img-20161004-wa0005
img-20161004-wa0006
img-20161004-wa0007
img-20161004-wa0008
img-20161004-wa0009
img-20161004-wa0010

0 comments:

Post a Comment