Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Tuesday, March 14, 2017

Ni ile Barabara Paul Makonda alizindua ujenzi wake kwa kuendesha Greda

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameendelea na mpango wake wa kubadilisha muonekano wa jiji la Dar es salaam kufikia viwango vya majiji ya kimataifa leo hii amegusa idara ya miundombinu ya barabara ambayo ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile.
Ombi la ujenzi wa miundombinu ya barabara ya bandari via kidongo chekundu yenye urefu wa km 1 ambayo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari hapa nchini lilitolewa na Paul Mkaonda miezi 2 iliyopita kwa kampuni ya ujenzi ya kizalendo ya Grant Tech Company, M kandarasi huyu amekabidhi barabara iliyokamilika kwa kiwango cha zege yenye zaidi ya thamani ya mil 750.

0 comments:

Post a Comment