Tuesday, December 20, 2016
CCM mkoa wa Dar es salaam imesema haifanyi maamuzi yake kwa kuangalia maoni ya wapinzani
Chama cha mapinduzi mkoa wa Dar es salaam kimesema halmashauri kuu taifa ya chama hicho hakifanyi maamuzi yake kwa kuangalia maoni ya wapinzani na wakosoaji wao kufuatia maadhimio ya mkutano wa halmashauri kuu taifa wa Desember 12 uliofanyika jijini Dar es salaam ambao ulipendekeza kupunguzwa kwa idadi ya wajumbe kutoka 358 hadi 158.
Akizungumza jijini Dar es salaam Katibu wa siasa na uenezi wa mkoa wa huo JUMA GADAFI amesema wapinzani wamekuwa na kawaida kukosoa kila jambo linalofanywa na chama hicho tawala bila kutambua juhudi zinayofanywa na serikali na kuongeza kuwa maamuizi hayo ni sahihi kwa kuwa yamefata taratibu za uendeshaji wa chama.
Aidha GADAFI ameeleza kuwa chama hicho kinaanza mchakato wa kushiriki uchaguzi mdogo kata ya KIJICHI kufuatia aliyekuwa diwani wake Charles Anderson kufariki Dunia ambapo sasa nafasi hiyo itawakirishwa na mgombea wa kike FAUSTA KILOMO katika uchaguzi utakaofanyika january 23 mwakani.
Chama hicho pia kimempongeza Rais Magufuli ambae pia ni mwenyekiti wa CCM taifa kwa mafanikio mbalimbali ikiweno kuziba nafasi za uongozi kwa kumteua aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya ubungo HAMPHREY POLEPOLE kuwa katibu wa itikadi na uenezi taifa.
0 comments:
Post a Comment