Thursday, November 3, 2016
Lwakatare amuangukia JPM
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/3439240/highRes/1479424/-/maxw/600/-/14dorrd/-/Magufuli.jpg
Ikiwa imepita takriban miezi miwili tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred Lwakatare amemlilia Rais Dk John Magufuli akitaka afike kujionea maafa yaliyowakumba wananchi na kusababisha madhara makubwa ya kibinadamu.Mbunge wa Bukoba Mjini (Chadema), Wilfred
Tetemeko hilo lilitokea Septemba 10 na kusababisha vifo vya watu 17, kujeruhi zaidi ya watu 200 na uharibifu wa nyumba zaidi ya 3,000 pamoja na miundombinu mbalimbali.
Viongozi mbalimbali wa nchi wakiongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa walifika katika mkoa huo huku misaada mbalimbali ikitolewa, lakini Lwakatare amemuomba Rais Magufuli afike na kujionea maafa hayo.
Lwakatare alitoa kauli hiyo juzi jioni wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2017/18.
0 comments:
Post a Comment