Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, October 6, 2016

VIDEO YA WALIMU WAKIMSHUSHIA KIPIGO MWANAFUNZI OFISINI YAZUA GUMZO MTANDAONI,KUNA HII TAARIFA KUTOKA KWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI

Video hii ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia leo alfajiri inawaonyesha walimu wakichangia kumpiga mwanafunzi mmoja ndani ya ofisi.



Walimu hawa wanaonekana si tu wanampiga mwanafunzi huyo kwa viboko, bali wengine wanampiga makofi ya uso, huku walimu wengine wakiwasihi wamuache mwanafunzi huyo kwani wanaweza kumuumiza.



Inadawa shule hii ni Mbeya Day, iliyopo jijini Mbeya..

Kuna hii taarifa mtandaoni katika ukurasa wa Facebook wa waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba

Taarifa rasmi za tukio la kupigwa Mwanafunzi
Mnamo Tarehe 28.9.2016, mwanafunzi aitwaye Sebastian Chinguku wa form 3A mbeya day sec school aishie Uyole alipigwa na walimu watatu, Mwl Frank Msigwa, John Deo UDSM na Sanke Gwamaka wa Nyerere Memorial, wote wakiwa mafunzo. 

Mwl Frank alitoa assignment ya Kingereza na baadhi ya wanafunzi hawakufanya akiwepo Sebastian hakufanya, darasani mwl alimpiga kofi kijana na kijana akahoji kwanini anampiga wakashikana koo, ndio walimu wakamchukua na kumpeleka staff room na kuanza kumpiga vile. Tangu tar 29. September mwanafunzi hakuonekana shuleni. 

Na mwl E.H wa Iringa University ndio aliyekuwa akisema mwacheni mtamuumiza. Ndio aliyechukua video. Hao walimu wote hawapo wameondoka kwenda kwenye vyuo vyao. POLISI wanaendelea kuwahoji uongozi wa Mbeya Day Sec School na Mwanafunzi aliyeumizwa ikiwepo kumpeleka hospitali.

Nimeelekeza vyombo vya dola Dar wawatafute chuoni kwao hao walimu kuhusiana na shambulio hilo kwa mwanafunzi huyo. MWIGULU Nchemba, W MNN"

VIDEO IPO HAPO CHINI;

https://youtu.be/rZRBYDX1ZLg

0 comments:

Post a Comment