POLISI mkoani Rukwa inawashikiliwa watu
wawili akiwemo mwanaume anayedaiwa kumbaka na kumyonga mjamzito Beatrice
Kalula (34) mkazi wa kitongoji cha Ichese , Bonde la Ziwa Rukwa
wilayani Sumbawanga.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Rukwa ,George Kyando amesema, mwanaume huyo Adrian
Maliati (30) na Ester Mwandila (30) walishirikiana kumshambulia na
kumnyonga mjamzito huo.
Amesema mtuhumiwa mwingine aliyefahamika kwa jina la Mama Gulo ametoroka baada ya tukio hilo, anatafutwa.
Kwa
mujibu wa Kyando, mkasa huo ulitokea Oktoba 4, mwaka huu saa 3:00
asubuhi katika kitongoji cha Ichese, Kata ya Mtowisa, Bonde la Ziwa
Rukwa wilayani Sumbawanga.
Imedaiwa
kuwa baada ya mwanaume huyo kumbaka mjamzito huyo alishirikiana na
wanawake hao wawili kumshambulia kisha kumnyonga na mwili wake
kuutelekeza kwenye shamba la Job Malingumu.
“Mwili
wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi katika kituo cha Afya cha Mtosiwa
ulikuwa na jeraha jicho la kulia, michubuko shingoni na damu zilikuwa
zikitoka kwa wingi sehemu zake za siri, Chanzo cha mauji hayo bado
hakijafahamika ambapo watuhumiwa hao wawili watafikishwa mahakamani"
amesema.
Imeandikwa na Peti Siyame- Habari leo Sumbawanga
0 comments:
Post a Comment