Mfanyabiashara kutoka Nigeria Aliko Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa mujibu wa orodha ya mabilionea mwaka 2017 iliyoandaliwa na jarida la Forbes.
Utajiri wa Dangote unakadiriwa kuwa jumla ya $12.2 bilioni.
Kuna mabilionea (wa Dola) 25 mwaka huu barani Afrika, mmoja juu ya 24 waliokuwepo mwaka jana.
Wafanyabiasha kutoka Nigeria Femi Otedola na Abdulsamad Rabiu hawakufanikiwa kuingia kwenye orodha hiyo mwaka huu.
Mtanzania Mohammed Dewji bado ndiye bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika, utajiri wake ukikadiriwa kuwa $1.09 bilioni.
Isabel dos Santos kutoka Angola na mfanyabiashara wa mafuta Folorunsho Alakija kutoka Nigeria ndiye mabilionea wanawake pekee katika orodha hiyo mwaka huu.
Bw Dangote Dangote, ndiye mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Dangote Cement inayoongoza kwa kuzalisha saruji Afrika. Anamiliki asilimia 90 ya hisa za kampuni hiyo.
Dangote Cement huzalisha tani 44 milioni za saruji kila mwaka na imepanga kuongeza uzalishaji kwa asilimia 33 kufikia 2020.
Dangote pia anamiliki hisa katika kampuni za chumvi, sukari na unga.
Mohammed Dewji ni afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya METL iliyoanzishwa na babake miaka ya 1970. Kampuni hiyo huhusika katika biashara ya nguo, unga, vinywaji na mafuta. Kampuni hiyo huendesha shughuli zake katika zaidi ya mataifa sita barani Afrika.
Mabilionea 25 wa Afrika mwaka 2017:
1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni
9. Isabel dos Santos, Angola
Utajiri: $3.1 bilioni
10. Issad Rebrab, Algeria
Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni
18. Folorunsho Alakija, Nigeria
Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni
20. Mohammed Dewji, Tanzania
Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni
Tuesday, March 21, 2017
Forbes: Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017
Tuesday, March 14, 2017
Mbwa tumika kugundua saratani ya tezi dume
Shirika la afya Uingereza “NHS” limesema hivi karibuni wataanza kutumia Mbwa kugundua saratani ya tezi dume ambayo huwaathiri zaidi wanaume kuanzia miaka 50. Kwa mujibu wa utafiti kwa zaidi ya asilimia 93 mbwa huweza kugundua cancer hiyo kwa kunusa mkojo wa mtu anayeugua saratani hiyo .
Akizungumza na CNN mbunge Jeremy Hunt alisema……. >>>‘ni vizuri kuangalia na njia zingine katika kufanya mambo na si lazima kila muda kutegemea sayansi na wataendelea kuangalia usahihi wa mbwa katika kugundua saratani hiyo na kuipa nafasi’.
Kutumika kwa mbwa katika kugundua magonjwa mbalimbali si jambo geni ambapo mwaka 2016 ili ripotiwa Mtoto wa miaka wa 13 kutumia Mbwa wake kugundua ugonjwa wa kisukari na mwaka 2009 Mbwa alitumika kugundua saratani ya matiti
Monday, March 13, 2017
Njia sita za jinsi furaha inavyoweza kuimarisha afya yako
Zipo sababu nyingi zimetajwa kuwa zinaweza kumfanya mtu aishi kwa furaha ambazo ni pamoja na kuamini katika kipato chako; kudumisha amani ya moyo huku ikitajwa furaha hiyo kuwa ni moja ya sababu zinazoweza kukufanya uwe na afya nzuri.
Leo nimekutana na hii ya njia sita ambazo furaha inaweza kuimarisha afya yako.
1: Furaha uulinda moyo wako
Utafiti unaonesha kuwa asili ya upendo na furaha siyo moyoni lakini husaidia kuulinda huku ikibainika kuwepo kwa uhusiano baina ya furaha na vipimo vingine vya afya ya moyo kama vile muda unaotumika wakati wa pigo moja la moyo na lingine na kuzilinganisha na hatari kadhaa za magonjwa ya moyo.
2: Furaha huimarisha mfumo wa kinga mwilini
Utafiti unaonesha kuwa mfumo wa kinga ya mwili hupanda na kushuka kutegemea na furaha aliyokuwa nayo mtu ambapo kuna uhusiano mkubwa baina ya furaha na mfumo imara wa kinga.
3: Furaha huzuwia mkazo (stress)
Mkazo (stress) hausababishi matatizo ya kisaikolojia pekee bali pia husababisha mabadiliko ya ki-biology katika homoni zetu na shinikizo la damu. Furaha inatajwa kupoza hasira za athari hizi na wakati mwingine kutusaidia kurudi katika hali ya kawaida kwa haraka.
4: Watu wenye furaha hawaumwi mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu
Watu ambao wana mood nzuri wana nafasi nzuri sana ya kuimarisha furaha ambayo huwasaidia kutoumwa homa za mara kwa mara na huwa na kiwango kidogo cha maumivu tofauti na watu ambao wana mood mbaya.
5: Furaha huzuia magonjwa na ulemavu
Furaha inatajwa kuhusika katika kuboresha hali ya makali ya homa za muda mrefu na mfupi na maumivu.
6: Furaha hurefusha maisha
Watu wenye furaha huweza kuishi kwa miaka 7-10 zaidi tofauti na wasiokuwa na furaha. Katika utafiti uliofanywa kwa wazee 4,000 wa Uingereza wenye umri wa miaka 52-79 ambao walikuwa na furaha mara nyingi zaidi kwa siku na kuonesha kuwa watu wenye furaha walikuwa chini ya 35% kufa ukilinganisha na watu ambao hawakuwa na furaha.
Saturday, March 11, 2017
Tujifunze mbinu za kuondokana na umasikini katika jamii yetu
Kuna baadhi ya watu mbalimbali waliweza kueleza maana ya umaskini kutokana na wao wanavyoelewa. Wapo baadhi ya watu walisema kuwa umaskini hutokana mtu kuishi chini ya dola moja kwa siku. Wapo pia waliosema kuwa neno umaskini halina maana sahihi kutokana na kila msomi alivyokuwa na tafsiri yake.
Tuachane na hayo na kuacha kila mmoja aweze kubaki na maana ambayo kila mmoja aweze kuelewa mwenyewe kutoka na anavyoona jinsi maisha yake na jamii kwa ujumla. Fuatana nami katika muda huu ili uweze kujua mbinu za kuondokana na umaskini hadi utajiri.
Zifuatazo ndizo mbinu za kuondokana na umaskini hadi utajiri.
1. Kuondokana na dhana potofu.
Moja ya changamoto ambayo inatukumbuka wengi ni kuishi katika kuamini ya kwamba ni lazima ujihusishe na masuala ya kishirikina ili ufanikiwe zaidi. Misingi hiyo endapo utaishi nayo na kukua nayo itakufanya uamini ya kuwa maisha ya mafanikio hayapatikani kwa njia njia nyingne isipokuwa ushirikina. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya kweli yanapatikana kwa wewe kufanya kazi kwa bidii.
Kila jambo linahitaji juhudi za kiutendaji na si vinginevyo. Mafanikio yanayopatikana kwa njia ya ushirikina ni njia ya mkato yenye madhara makubwa ndani ya muda mfupi kama unabisha jaribu kufanya hivyo uone. Ukitaka kufanikiwa zaidi jambo la msingi ni kufikiri mara mbili na kwa umakini wa hali ya juu huku ukibadili mtazamo .
Ondokana na dhana potofu zinazokuzuia kupata pesa.
2. Kujiamini kwa jambo lolote.
Kwa kuwa wewe ndiye msaka tonge kwa kutumia mbinu halali za kimafanikio huku ukiongeza juhudi na ubunifu katika utendaji wako wa kazi huku ukiamini ya kwamba wewe ni zaidi ya watu mabilionea. Unajua kwa nini nimesema hivyo? ni kwa sababu wengi wetu hatuamini katika kazi ambazo tunazifanya.
Ukichunguza kwa umakini tofauti kubwa kati ya maskini na tajiri utagundua katika kauli zao. Maskini akiwa anaenda kufanya kazi zake utashangaa wakati anaaga utamsikia naenda kuhangaika. Au ukimpigia simu ukimuuliza upo wapi kwa sasa utamsikia nipo kwenye mihangaiko tu ndugu yangu. Wakati kwa upande wa tajiri huwa ni kinyume chake ukimuuliza upo wapi atakwambia nipo kazini.
Na asubuhi utamsikia naenda ofisi.
Ukichunguza kwa umakini katika kauli hizo utagundua ya kwamba maskini ni mtu wa kutojiamini hata kidogo wakati wewe una uwezo wa kutengeneza kipato zaidi ya huyo anayesema naenda kazini.
Ewe Msomaji wa makala haya endapo utaendelea na kauli zako hizo ya kwamba naenda kwenye mihangaiko ni kweli utahangaika mpaka pumzi itapokata hivyo ni wakati wako sahihi wa kubadili kauli zako kwa kusema huku unajiamini, na wewe unaenda kazini na ofisini.
3. Kubali kukosolewa.
Huwa nafurahi sana hasa pale tunapokutana na marafiki zangu tukiwa tunazungumzia mchezo wa mpira wa miguu. Huwa tunakuwa na hoja mbalimbali na kusema fulani kabebwa, huku wengine wakisema yaani leo kocha angemchezesha fulani ingewezekana tungeshinda.
Unajua ni kwa nini nimekupa kisa hicho ukweli ni kwamba watu wanakuzunguka ni wazuri sana katika kugundua jambo ambalo unalolifanya kwa kuona mapungufu na mazuri iliyonayo. Hivyo ni muda wako sahihi wa kuchukua maoni yao na kuweza kuyafanyia kazi ili kuweza kuboresha ofisi au jambo lako.
Ewe msaka Mafanikio kumbuka ya kwamba tumia kidogo ulicho nacho ili kupata mafanikio zaidi.
Friday, March 10, 2017
PICHA3: Jinsi sanamu la Mfalme Farao II aliyetawala miaka 3000 lilivyopatikana
March 9 2017 imeripotiwa taarifa kutokea Misri kuhusu Sanamu ya mfalme Farao II, sanamu hilo limepatikana chini ya Ardhi na inasemekena ni la Mfalme Farao Ramses II aliyetawala Misri zaidi ya miaka 3,000 iliyopita lenye Mita 8 (26 ft) , Sanamu hilo limegunduliwa na wanasayansi kutoka Misri na Ujerumani.
Farao pia alijulikana kama Ramses na alitawala Misri kwa miaka 66, kutoka 1213BC hadi 1279BC
Saturday, March 4, 2017
Mti wenye umri wa miaka 600 wapatikana moshi
Mtafiti wa viumbe hai na mazingira kutoka Chuo Kikuu cha Bayreuth cha nchini Ujerumani, Dk Andrew Hemp ameelezea sifa za mti ujulikanao kama Mkukusu kuwa unaweza kuishi kati ya miaka 200 hadi 300, lakini ulioonekana nchini una miaka 600.
Akiuzungumzia mti huo ambao unapatikana katika Kijiji cha Tema wilayani Moshi, mtafiti huyo amesema mti huo ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika una urefu wa mita 81.5 na uko katika eneo lililopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa).
Dk Andrew amesema kwa mujibu wa utafiti mti huo una uwezo wa kuishi miaka hiyo kwa kutunzwa na kuhifadhiwa.Amesema kwamba katika utafiti walioufanya barani Afrika waligundua miti mirefu 31, lakini Mkukusu wa Moshi ndiyo mrefu kuliko yote na una umri wa miaka 600 hivi sasa ukiwa umevuka kiwango cha juu cha maisha ya miti ya aina hiyo.
Tayari Serikali imeiagiza Kinapa kuboresha miundombinu ya barabara ili kuweza kuufikia mti huo iwapo watalii watataka kwenda kuuona.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki amesema mti huo utasaidia kuongeza mapato kwa kasi kwa kuwa ni kivutio kipya cha utalii ndani ya mkoa huu.
Monday, February 27, 2017
Zingatia Haya Kabla Ya Kufanyia Kazi Ushauri Wa Kibiashara Unaopewa
Kama kuna kitu ambacho kila mtu anaweza kushauri kadiri ya utashi wake, basi ni ushauri wa kibiashara. Watu wengi wamekuwa wakipokea ushauri wa biashara unaotolewa na kila mtu, tena kwa bure, lakini wanapoufanyia kazi ndipo wanagundua haukuwa ushauri mzuri.
Kila kipindi kuna aina za biashara ambazo huwa zinashabikiwa na watu wengi, biashara ambazo kila mtu anaongelea na wale wanaozifanya kuonekana waipata faida. Hapa ndipo unakuta kila mtu anashauriwa kuingia kwenye biashara hiyo, kwa sababu ndiyo ‘habari ya mjini’ kwa wakati huo na hivyo wengi wanakimbilia kuchukua hatua kabla fursa haijawapita.
Changamoto nyingine kubwa inayowafanya watu kupewa ushauri ambao siyo makini kwenye biashara ni kutokuwa tayari kulipa gharama za ushauri. Wengi wamekuwa wakichukulia ushauri kama kitu kidogo ambacho hakipaswi kulipiwa. Hivyo wanachukua ushauri wa bure ambao unawaumiza sana.
Leo tutakwenda kujifunza mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kufanyia kazi ushauri wowote unaopewa kibiashara. Kwa kuzingatia mambo haya utaepuka kufanya maamuzi ya msukumo ambayo yatakuingiza kwenye hasara.
Jambo la kwanza; fanya utafiti wako mwenyewe.
Usipokee maneno ya watu na kuyaamini kwa asilimia mia moja. Fanya utafiti wako kujua kama kweli biashara unayoambiwa inalipa kama ni kweli. Angalia ukubwa wa soko la biashara hiyo, ona ni kwa kiasi gani bado wateja hawajafikiwa. Pia angalia uwezekano wa kukua zaidi kwenye biashara hiyo. Fanya utafiti wako mdogo kulijua soko na hata kuwajua wale waliopo kwenye biashara hiyo kwa sasa.
Jambo la pili; ongea na wale wanaofanya.
Kwa kuwa umesikia biashara inalipa, usifikiri kwamba haina changamoto zake. Na ili kujua changamoto za biashara yoyote, angalia wale ambao wanafanya biashara hiyo. Ongea nao au wafuatilie ili kuona changamoto yao hasa ni nini. Ni vyema ukazijua changamoto za biashara yako mapema kabla hata hujaingia ili uweze kupambana nazo.
Wengi wa wanaoshindwa kwenye biashara mpya ni kutokana na kukutana na changamoto ambazo hawakuzitegemea hapo awali.
Jambo la tatu; mwangalie yule anayekupa ushauri wa biashara.
Watu wengi wamekuwa wakitaka kusikia tu ushauri mzuri wa biashara, hivyo wakiusikia hawajali anayewaambia ni nani. Hivyo unakuta mtu kasikia wengine wanasema biashara fulani inalipa, na yeye anatoka na taarifa hizo kuja kukupa wewe. Hajafanya utafiti wowote na wala hana utaalamu wa biashara, ila amesikia inalipa na anakuambia na wewe ukafanye kwa sababu inalipa.
Hakikisha mtu unayechukua ushauri wa biashara kwake ana utaalamu wa biashara au anafanya biashara hiyo anayokushauri ufanye. Kama na yeye amesikia inalipa ila hajui kwa kina kuhusu biashara hiyo, ni vyema ukaokoa muda wako au kufanya utafiti zaidi kabla hujaingia kwenye biashara hiyo.
Ni rahisi kushauri kuliko kufanya, hivyo mara zote unapopokea ushauri chunguza kwa makini kabla hujachukua hatua. Usiharakishe kufanyia kazi ushauri unaopewa kwa sababu tu unaonekana ni biashara itakayokulipa. Fanyia kazi ushauri unaopewa na utoke na mpango ambao unaweza kuupigania mpaka kufanikiwa kwenye biashara yako.
Wednesday, February 22, 2017
Wanasayansi wagundua sayari saba sawa na dunia
Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.
Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.
Hata hivyo wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.
Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwa
Mambo muhimu kuhusu sayari ya Mars
Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi
"Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta 'dunia ya pili', na kwamba sasa si jamba la kusema kama ingelikuwa hivi, bali sasa tunasema ni lini. Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu, nne, tano hadi saba, jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale,'' amesema Zurbuchen.
Michael Gillion ni mmoja wa wanajopo hilo la wana sayansi kutoka chuo kikuu cha anasema sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo na zina sifa tofauti.
"Inaonyesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, chakushangaza zaidi ni kwamba maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo," amesema Gillion.
Kemikali inayounda sehemu ya ndani ya dunia
Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika anga hillo kuna nini.
Hata kuzifikia sayari hizo ni mtihani mwingine wani umbali wake hata mwendokasi wa mwanga, unaoongoza hapa duniani kwenda kwa haraka, unaweza kuzifikia sayari hizo baada ya miaka 40
Utafiti: Wanawake Korea Kusini kuishi miaka mingi zaidi duniani
Wanawake nchini Korea Kusini watakuwa wa kwanza duniani kuwa na umri wa kuishi wa zaidi ya miaka 90, utafiti unaonesha.
Utafiti huo uliofanywa na Chuo cha Imperial cha London na Shirika la Afya Duniani uliangazia umri wa kuishi katika mataifa 35 yaliyostawi kiviwanda.
Utafiti huo unaonesha watu watakuwa wakishi miaka mingi kuliko sasa kufikia mwaka 2030 na pengo kati ya wanaume na wanawake litaanza kufutika katika mataifa mengi.
Watafiti hao wanasema matokeo ya utafiti wao ni changamoto kwa hazina za malipo ya uzeeni na vituo vinavyowatunza wazee.
"Korea Kusini imefanya mambo mengi kwa njia ifaayo," Prof Majid Ezzati aliambia BBC.
"Wanaonekana kuwa na mazingira yenye usawa na mambo yao mengi yamewafaa watu kwa juma - elimu, lishe - watu wengi wamenufaika.
"Na kufikia sasa, wanafanya vyema katika kukabiliana na shinikizo la damu na wana viwango vya chini zaidi vya unene duniani."
Takwimu hizo pia zinakadiria kwamba Japan, ambayo zamani ilifahamika kwa raia wake kuishi maisha marefu, inaendelea kushuka.
Kwa sasa, ina kiwango cha juu zaidi cha umri ambao wanawake huishi, lakini itapitwa hivi karibuni na KOrea Kusini na Ufaransa, utafiti huo unadokeza.
Umri wa wanaume kuishi Japan nao utashuka kutoka kuwa wa nne miongoni mwa nchi zilizochunguzwa hadi nambari 11.
Marekani yabaki nyuma
Marekani pia haijafanya vyema kwa mujibu wa utafiti huo na huenda ikawa na kiwango cha chini zaidi cha umri wa kuishi miongoni mwa mataifa tajiri kufikia 2030.
Utafiti huo unabashiri kwamba kiwango cha wastani cha umri wa wanaume kuishi Marekani kitakuwa miaka 80 kwa wanaume na 83 kwa wanawake, karibu sawa na Mexico na Croatia wakati huo.
Marekani pia itakuwa imepitwa na Chile, ambapo wanawake watakaozaliwa 2030 watatarajia kuishi miaka 87 na wanaume 81.
Kati ya 2015 na 2030, umri wa kuishi Uingereza utapanda kutoka 79 hadi 82 kwa wanaume na 83 hadi 85 kwa wanawake.
Wanaume wanapanda
Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la Lancet, unaonesha pengo kati ya umri wa kuishi kati ya wanawake na wanaume linapungua.
Prof Ezzati alisema: "Wanaume kawaida waliishi maisha yasiyo ya afya, na hawaishi muda mrefu ukilinganisha na wanawake. Walikunywa pombe na kuvuta sigara zaidi, na waliuawa sana nyumbani au kufa kwenye ajali barabarani. Hata hivyo, mtindo wa maisha kati ya wanaume na wanawake sasa unakaribia kufanana. Hivyo, umri wa wanaume kuishi unaonekana kuongezeka."

