Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads
Showing posts with label BIASHARA. Show all posts
Showing posts with label BIASHARA. Show all posts

Wednesday, February 22, 2017

Mafuta ya kupikia yapanda bei

BEI ya mafuta ya kupikia imepanda kutoka Sh 2,500 kwa lita hadi Sh 3,500 MTANZANIA limebaini.
Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA jana katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam umebaini kuwa lita moja ya mafuta ya kula imeongezeka, huku ndoo ya lita 20 ikiuzwa kati ya Sh 55,000 na 60,000 badala ya Sh 52,000.
Katika maeneo ya Tandale na maduka yaliyopo katika mitaa ya Sinza na Manzese, ongezeko hilo limeongeza ukali wa maisha kwa watu wengi hasa wa hali ya chini kutokana na kuendelea kupanda kwa bei ya vyakula inayochagizwa na ukame katika mikoa mbalimbali nchini.
Soko la jumla la Tandale, mchele unauzwa kwa bei ya jumla kati ya Sh 200,000 na 220,000 kwa gunia moja lenye kilo 100, huku kilo moja ikiuzwa kati ya Sh 2,400 na 2,500.
Mahindi yamepanda kutoka wastani wa Sh.120,000 hadi 180,000 kwa gunia moja la kilo 100, huku kilo moja ya mahindi ikiuzwa kwa Sh. 2,000.
Mfuko wa unga wa mahindi wenye kilo 25 ambao awali ulikuwa ukiuzwa kwa Sh 22,000 na baadaye uliuzwa  kwa Sh 35,000 hivi sasa unauzwa Sh 40,000 na kilo moja ikiuzwa kwa Sh 2000 badala ya Sh 1500.
Maharage gunia moja linauzwa Sh 200,000 hadi 250,000 kulingana na ubora wake, wakati kilo moja inauzwa Sh 2,600 hadi Sh 3,200.
Akizungumzia kupanda kwa bei hizo, mmoja wa wateja wa bidhaa hizo, Neema Mmbaga alisema familia yake imebadili mfumo wa kula ambapo hivi sasa wanakula mara moja kwa siku.
“Inatubidi kula mara moja kwa siku kutokana na upatikanaji wa fedha kuwa mgumu na vyakula kuendelea kupanda kila kukicha,” alisema Neema.

Friday, February 17, 2017

Magari yanayotumia umeme kuathiri biashara ya mafuta ndani ya miaka 10

Suala la magari yanayotumia umeme kuathiri biashara ya uchimbaji na uuzaji mafuta miaka 2-4 iliyopita lisingeonekana kama ni tishio sana, ila sasa watafiti wanasema hivyo. Ndani ya miaka hii miwili teknolojia ya magari yanayotumia umeme imekua sana. Makampuni mengi yamewekeza katika teknolojia hiyo na hivyo kusababisha ata bei ya magari hayo kushuka kwa kiasi kikubwa. Kituo la masuala la utafiti chini ya chuo kimoja nchini London – Carbon Tracker Initiative and Imperial College London, kimesema kutakuwa na upungufu wa uhitaji wa mafuta takribani mapipa milioni 2 kwa siku kufikia mwaka 2025. Soko hilo litapotea kutokana na ukuaji wa ununuaji na utumiaji wa magari yanayotumia teknolojia ya kuendeshwa na umeme. Ripoti hiyo inasema hadi kufikia mwaka 2050 upungufu wa uhitaji utafikia mapipa milioni 25. Hii inamaanisha mataifa yanayotegemea biashara ya mafuta yanayotumika katika uendeshaji wa injini za magari yataathirika sana. Na pia kutokana na ukuaji wa manunuzi ya magari haya basi tutazidi kuona bei ya mafuta ikizidi kushuka kutokana na ushindani. Bei? Bei ya magari yanayotumia umeme yamezidi imezidi kushuka katika mataifa kama Marekani na kila makampuni mengine mengi ya magari yakizidi kuwekeza kwenye magari hayo bei inazidi kuwa sambasamba na ya magari yanayotumia mafuta. Inategemewa kufikia mwaka 2025 magari yanayotumia umeme yatakuwa asilimia 35 ya magari yanayotumika wakti hadi mwaka 2050 itafikia takribani asilimia 66 ya magari yote.

Tuesday, November 15, 2016

Wakulima Tunduru wapata soko la korosho

WAKULIMA wa korosho Wilaya ya Tunduru, wameondokana na umasikini kutokana na kupata soko la uhakika baada ya Kampuni ya Namela General Trade kushinda zabuni ya kununua zao hilo wakulima kwa bei ya Sh 3,757 kwa kilo, ikizishinda kampuni nyingine saba. Hadi kufikia Novemba 14, kulikuwa na zaidi ya tani 541 zilizoingizwa katika ghala la Chama Kikuu cha Ushirika Wilaya ya Tunduru (Tancu) ambako kampuni hiyo ilipewa kununua korosho tani 400 huku Kampuni ya Machinga iliyoshinda nafasi ya pili katika mnada huo, ikipata kibali cha kununua tani 141 kwa bei ya Sh 3,750. Juzi, Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma, iliingia katika historia mpya tangu ianzishwe mwaka 1905, kwa wakulima kuuza zao hilo kwa njia ya mnada, jambo liliwafurahisha wakulima na wananch wengine. Kampuni zilizoomba kununua korosho kwa njia ya mnada wilayani Tunduru zilikuwa saba, Namela iliomba kununua tani 400,000 kwa bei ya Sh 3,757, Machinga tani 400,000 kwa bei ya Sh 3,750, ETC Ltd ilitangaza bei ya Sh 3,700, Vikat Ltd 250,000 kwa bei ya Sh 3,277, Maviga East Africa tani 400 kwa Sh 3,500, na kampuni nyingine mbili ambazo ziliomba kununua kwa bei ya chini. Akizindua mnada huo uliofanyika katika viwanja vya Tancu, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera amewataka wananchi wa Tunduru kuwa na imani na serikali yao ya Chama Cha Mapinduzi ambayo imeonesha dhamira ya dhati kuwakomboa wananchi na maadui watatu ambao ni umaskini, ujinga na maradhi. Homera amewataka kuendelea kuiunga mkono serikali wakati huu ambao imejipanga kuhakikisha inaondoa vitendo vya dhuluma, wizi na mambo mabaya ambayo kwa muda mrefu yamekuwa kero kwa Watanzania. Aidha, amewakumbusha wakulima wa korosho kujiwekea akiba na kutumia fedha hizo katika mambo ya msingi, badala ya kuzielekeza katika anasa, jambo linaloweza kuwarudisha nyuma. Ametoa siku tatu kwa kampuni zilizoshinda kuanza malipo ili wakulima ajiandae na msimu mpya wa kilimo mashambani. Meneja Mkuu wa Tancu, Iman Kalembo alisema kazi ya kukusanya korosho kutoka katika vyama vya msingi vya ushirika ilianza tangu Septemba, lakini walishindwa kuanza mnada mapema kutokana na changamoto mbalimbali kama vile uhaba wa magari ya kubeba zao hilo kutoka shambani hadi kwenye maghala

Sunday, November 13, 2016

Tanzania Kupata Bilioni 12 Za Trademark East Africa Kusaidia Wafanyabiashara Wanawake

Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania (TWCC) jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Tanzania itafaidika na msaada wa Dola za Marekani Milioni 5,300,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Kitanzania, zitakazotolewa na Taasisi ya TradMark, East Afrika, kuwajengea uwezo wafanyabiashara wanawake wa Tanzania, kuyafikia masoko ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hata nje ya Afrika na kwa kuanzia, TradeMark, itaanzisha madawati ya jinsia kwenye mipaka mitatu ya Holili, Kabanga na Mutukula. Ahadi ya fedha hizo, imetolewa na Mkurugenzi wa TradeMark Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga (pichani), wakati akifungua Mkutano wa Chama cha Wafanya Biashara Wanawake wa Tanzania, TWCC, kujadili vikwazo kwa wafanyabiashara wanawake mipakani, uliofanyika jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Ulanga amesema fedha hizo zitatolewa na TradeMark East Africa, kupitia mradi wake wa “Women in Trade” uliolenga kuwajengea uwezo kuhimili ushindani wa kibiashara na kukabiliana na vikwazo vya kibiashara kwa wafanyabiasha wanawake Tanzania kuwawezesha kufanya biashara ya kimataifa ikiwemo kuwezesha bidhaa zao kuyafikia masoko ya nchi za Afrika Mashariki na soko la kimataifa. Bwana Ulanga amesema, TradeMark East Africa ni taasisi inayoongoza katika kuleta usawa wa kijinsia katika biashara, kwa sababu utafiti umeonyesha kuwa asilimia 70% ya wanaofanya biashara za mipakani ni wanawake na wanakabiliwa na vikwazo vingi vya kibiashara vikiwemo vikwazo vya kijiografia, vikwazo vya kijinsia, vikwazo vya kisheria, vikwazo vya kimtazamo, hivyo TradeMark imeandaa mpango kamambe wa miaka sita wa kuwajengea uwezo, atakaogharimu shilingi bilioni 12, kati ya hizo, Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, TWCC, kitapatiwa shilingi milioni 500. Akishukuru kwa msaada huo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC), Bibi Jaquiline Mneney Maleko, ameishukuru TradeMark kwa msaada huo, na kuahidi utatumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa. TradeMark East Africa (TMEA) ni shirika lisilo la kiserikali, la maendeleo kwa lengo la kuongezeka ustawi wa kiuchumi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa njia ya biashara. TMEA inafanya kazi kwa karibu na taasisi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), serikali za kitaifa, sekta binafsi na asasi za kiraia. TMEA inachangia ukuaji wa biashara Afrika Mashariki kwa kufungua fursa za kiuchumi kupitia: • Kuongezeka kwa fursa za upatikanaji wa masoko; • Kuboresha mazingira ya biashara; na • Kuboresha biashara ya ushindani. Kuongezeka kwa kiwango cha biashara kuchangia ukuaji wa uchumi, na kupunguza umaskini na hatimaye kuongezeka ustawi. TMEA ina makao yake makuu mjini Nairobi nchini Kenya, na ina matawi katika miji ya Arusha, Bujumbura, Dar es Salaam, Juba, Kampala na Kigali. Ili kujua zaidi kuhusu TMEA, tafadhali tembelea tovuti TMEA katika www. www.trademarkea.com

Friday, October 7, 2016

AyoTV Tecno Phantom 6 kuanza kuuzwa, haya ni mambo ya kuyafahamu

Baada ya simu ya Tecno Phantom 6 na Phantom 6 plus kuzinduliwa usiku wa September 26 2016 huko Dubai kwenye jengo refu zaidi duniani, Burj Khalifa, October 8 2016 ndio siku pekee ya wewe mtu wangu kuweza kumiliki kifaa hicho kipya cha phantom 6 kwa kuinunua kwa mara ya kwanza hapa Tanzania katika viwanja vya City Mall Posta jijini Dar es Salaam. Simu hizo za Phantom 6 na phantom 6 plus zitakua na 32GB ROM, 3GB RAM na kamera mbili za nyuma zenye 13MP na 5MP, muonekano wa kuvutia pamoja na uwezo wake wa ajabu wa kuingiza chaji kwa haraka zaidi na kutunza chaji kwa muda mrefu. Vile vile mtu wangu ukiinunua Phantom 6 katika viwanja hivyo basi utapata nafasi ya kujishindia zawadi kem kem. Hizi ndizo zawadi ambazo unaweza kujishindia endapo utanunua phantom 6 kwa siku hiyo Kupata zawadi za TECNO kama T-Shirt, T-Band, begi na Selfie stick Kushiriki katika bahati nasibu na kupata nafasi ya kujishindia tiketi za kuangalia filamu, Winpad, Power bank na Kamera ya kupaa ( Drone) Kushiriki katika ulengaji wa puto na kupata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali droo Ndege hii ya kupaa itazawadiwa kwa mteja mmojawapo miongoni mwa wateja watakaojitokeza tarehe 8 Oktoba katika mauzo ya kwanza ya Tecno Phantom 6. Unaweza kupata taarifa zaidi kwa kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno. Facebook: https://www.facebook.com/TECNOMobileTanzania/?fref=ts Instagram: https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/ Twitter: https://twitter.com/TECNOMobileTZ

Thursday, October 6, 2016

Mbinu za Kupata Mtaji wa Biashara

Watu wengi wanatamani kumiliki biashara siku moja na huenda wana mipango mizuri juu ya bishara zao. Mipango hii inaweza ikawa vichwani tu au mingine katika maadishi lakini inapofika wakati wa utekelezaji wa mipango hii ukosefu wa mtaji wa biashara hiyo ni kipingamizi kwa wengi.

Lakini kuna jinsi kadhaa ambazo zinaweza kusaidia upatikanaji wa mitaji kwajili ya biashara.

 Aina Za Mitaji
Kuna aina mbili ya mitaji kwaajili ya biashara au uwekezaji wa aina yoyote.


  • Mtaji wa Mkopo
  • Mtaji wa Mmiliki

 Mtaji wa Mkopo unakuwezesha kukopa toka kwa taasisi za fedha au mtu binafsi wakiwemo ndugu ,jamaa na marafiki na kuhitajika kulipa katika kipindi maalumu ikiwa pamoja na riba au bila riba.

Aina hii ya mtaji inakuwezesha kufanya biashara lakini ni lazima uwe makini katika utunzaji wa fedha zako na uzalishaji wake kwani mwishowe utahitajika kurudisha fedha zote pamoja na riba pengine kila mwezi.

 Mtaji wa Mmiliki ni mtaji toka kwa mtu au kampuni ambayo inahitaji kuwa na umiliki wa sehemu ya bishara. Hawa wanataka kupata faida kutokana na uwekezaji katika kampuni au biashara yako.

Kama uko tayari kutoa sehemu ya umiliki wa biashara yako basi mtaji wa aina hii utakusaidia kuanzisha au kuboresha bishara yako.

Changamoto Za Kupata Mitaji:
Kupata mtaji wa biashara ni changamoto kubwa kwa wajasiriamali kote duniani. Japo fedha za mikopo zinapatikana katika mabenki lakini bishara nyingi hazina miundo mizuri na mifumo ya fedha kuwezesha kupata mikopo. Benki zimekuwa na masharti magumu sana kiasi kwamba bishara nyingi haziangalii huko kama sehemu ya kupata mikopo.

Mikopo toka kwa ndugu na jamaa pia ina changamoto zake,si rahisi ndugu au rafiki akakuamini au akaamini kuwa biashara yako itafanikiwa,tunajua asilimia 90 za biashara zinazoanza zinakufa kila mwaka. Hili linawapa wasiwasi sana wakopeshaji.

Mambo Ya Kuangalia Kabla Ya Kupata Mtaji



Mtaji Toka Kwenye Mikopo:
Ili kupata mikopo kunahitajika dhamana kuwahakikishia wakopeshaji wako kuwa kama hutafanikiwa basi ni kwa jinsi gani fedha zao zitarudi.

Na utakutana na msharti mengi magumu,dhamana inaweza kuwa kama ifuatavyo:

  • Nyumba
  • Kiwanja
  • Shamba
  • Gari
  • Mali za nyumbani au ofisini(biashara yenyewe)
  • Ni lazima ujiulize mapema kama uko tayari kuweka mojawapo ya vitu hivi kuwa dhamana.


Kwa namna hii ni rahisi kupata mkopo na ni lazima urudishe deni vinginevyo utapoteza.

Huu ndio ujasiriamali wenyewe, uthubutu wa kufanya mambo ya hatari katika harakati za kufanikiwa katika biashara.



Mtaji Toka Kwa Wawekezaji:
Kama utaamua kuingiza wawekezaji wengine katika biashara yako basi pia nilazima ufikirie mapema kuwa kutakuwa na taarifa ambazo watahitaji kujua juu ya mwenendo wa biashara yako.


  • Je unapata faida kwa sasa?
  • Muelekeo ukoje,unapanda na bidhaa au huduma zinahitajika?
  • Ni kwa namna ipi fedha zinzohitajika zitawekezwa ili kuboresha biashara na kuleta faida kwa haraka n.k
  • Waekezaji nao wanaangalia hatari ya kupoteza fedha zao na pia muda wa kurudisha fedha wanazowekeza na faida itakayozalishwa.


Kama biashara yako haiwezi kuonyesha haya kabla,ni ngumu kupata wawekezaji katika bishara yako.

Mpango Bishara na utunzaji mzuri wa mahesabu ya biashara yako yatasaidia sana kutoa taarifa hizi na hivyo kukusaidia kupata wawekezaji

Taarifa Za Fedha Na Mpango Wa Bishara Ni Nyenzo Muhimu Kupata Mtaji Wa Biashara
Kama ni niashara mpya ,kutahitajika kuwa na mpango wa biahsara,andiko ambalo linaelezea jinsi ambavyo biashara yako itafanyika ,kiasi cha fedha kinachohitajika, bidhaa na huduma utakazo toa ,masoko,na wafanyakazi.


Andiko hili litasaidia kushwawishi wawekezaji na watoa mikopo.
Kama biashara yako iko tayari na unataka kuongezea mtaji, basi utahitaji kuwa na taarifa za hali ya fedha ya bishara yako, pia unaweza ukaandaa mpango wa biashara unaoelezea mwelekeo wa biashara katika miaka kadhaa mbele.

Wafanyabishara wengi wa kati na wa chini hawafanyi haya, ndio maana kunakuwa na ugumu kupata mitaji ya kuanzia au kukuza biashara.

Huenda ukahitaji msaada toka kwa wataalamu wa biashara na upate usaidizi wa kitaalamu,andaa fedha kidogo kwajili ya huduma hizi. Kuna makampuni mengi tu sasa hivi ambayo yanatoa huduma kwa wafanyabiashara kwa gharama ndogo.

Mbinu 5 Za Kupata Mtaji Wa Biashara:
Aina hizi zote za kupata mitaji zinaingia katika makundi mawili yaliyotajwa hapo awali aidha ni mkopo au uwekezaji

1. Mkopo Toka Benki Au Tasisi Za Mikopo
Benki zote hutoa mikopo kwaajili ya biashara ila taarifa za muhimu zinahitajika kuhusu mwenendo wa biashara kama tayari imeshaanza au Mpango wa biashara unaoelezea jinsi ambavyo biashara itaendeshwa na jinsi ambavyo deni litalipwa.

Benki huhitaji vitu vya thamani kwajili ya dhamana ya fedha watakazokupa kama mtaji.

Iwapo fedha hazitarudishwa kama ambavyo iliwekwa katika masharti ya mkopo basi mali hiyo itauzwa ili kufidia deni.

Hili limekuwa ni changamoto kwa wengi kupata mikopo toka benki. Hasa kwa biashara anbazo zinaanza na hazina uhakika wa kufanya vizuri na uwezo wake wa kurudisha deni.

Aina hii ya mikopo inaweza ikawasaidia wale ambao bishara zao zimeshasimama na wanafanya kwa faida. Pia kwa zile biashara ambazo mzunguko wa fedha ni mkubwa na hawatahitaji muda mrefu wa kulipa deni.

Benki mpya mara nyingi huwa na msharti rahisi kuliko benki kongwe.
Aina nyingine ya mikopo ambayo inafanana na ile ya benki ni toka katika taasisi za mikopo. Taasisi hizi zinatoa masharti nafuu kido kuliko yale ya benki. Nchini Tanzania kuna tasisi maarufu kama FINCA,Blue ,Branc na nyingine nyingi ambazo zinatoa mikopo ya biashara.

Mara nyingine utahitaji kuwa katika vikundi ili kupata mikopo kwa urahisi au kuwa na biashara iliyosajiliwa kisheria.

2. Mkopo Toka Kwa Ndugu, Jamaa Au Marafiki
Ndugu na Marafiki ni sehemu nyingine ambayo unaweza kufikiria unapohitaji mtaji wa biashara.

Ni watu wanaokupenda na kukuamini na wako tayari kukusaidia katika harakati zako za kufanikiwa kibiashara. Wako tayari kukusaidia kama wana uwezo wakufanya hivyo. Lakini bado wanahitaji uhakika kuwa fedha zao zitarudi. Watapenda kujua mpango wako na ni lazima uwe tayari kuwajulisha,sio tu kabla hata baada ya kupata mkopo ili wajue mwenendo wa fedha zao.

Kumbuka dhamana hapa haitakuwa mali bali uaminifu wako kwao. Ukishindwa kufanya ulichoahidi utavunja uhusiano wenu mzuri uliojengeka kwa muda mrefu.

Ni vyema kufikiria kwa makini kama utahitaji kuchagua njia hii,vinginevyo si njia nzuri sana.


3. Toka Katika Vikundi Vya Kuweka Na Kukopa
Vyama vya Kuweka na Kukopa vinatoa mikopo kwa wanacama wake. Katika vyama hivi wanachama wanatakiwa kuweka fedha katika akaunti zao. Mwanachama anaruhusiwa kukopa kulingana na kiasi alichoweka. Baadhi ya vyama vinaruhusu mwanachama kuchukua mkopo kufikia mara nne ya kiasi alichoweka. Mkopo huu huwa na riba ndogo ulilinganishwa na benki.

Pia masharti yake si magumu na ya hatari kama ya benki.

Kuna vikundi vingine vya kijamii ambavyo wanachama wamekuwa wakifanya hivyo na vinatoa fursa kwa wanachama kupata mitaji kwa kukopa.

Vikundi vya Kuchangiana:
Pia kuna mtindo wa kuchangiana kila mwezi ambapo wanachama katika kikundi watachanga kiasi fulani cha fedha na kumpa mmoja wao ili afanya kitu fulani muhimu ambacho asingeweza kwa kuwekeza binafsi.


4. Mtaji Toka Kwa Wawekezaji Binafsi Wa Nje
Kuna watu binafsi na makapuni ambayo tayari yanafedha na yanahitaji kuwekeza katika biashara yenye kupata faida ili fedha zao ziongezeke. Watu hawa wanaweka fedha benki ambako hazizai kwa riba nzuri kulinganisha na biashara.

Watu hawa wanahitaji taarifa za kutosha kuwashawishi kuwa fedha zao ziko katika mikono sahihi. Pia hata baada ya kuwekeza watahitaji taarifa za mara kwa mara juu ya maendeleo ya biashara. Kama biashara ni mbaya huenda wakatoa fedha zao ili wasipate hasara.

Hii ni sehemu nyingine ambayo huwa haiangaliwi sana na wajasiriamali wadogo kwani ile dhana ya kufanya biashara kwa kushirikiana bado haijakubalika na kufuatwa. Lakini njia hii inatoa nafasi kwa wale ambao wanabiashara yenye mfumo mzuri na inakosa mtaji tu kufanikiwa.

Lakini hata kwa biashara zinazoanza, kama kuna mpango mzuri na wazo lenyewe la bishara linaonyesha kufanikiwa basi wawekezaji hawa watakuwa tayari kuwekeza katika biashara yako.

Hii ni njia nzuri kwa wale wenye uwezo wa kubuni biashara nzuri zenye kutoa huduma kwa watu na yenye nafasi kubwa ya mafanikio lakini wanakosa fedha za kuanzia. Hawa wanaweza wakaanza hata bila kuwa na shilingi moja,mpango wa biashara pekee ndio wanachohitaji.

Kisha ongea na matajiri katika mji wako(angalia usitoe taarifa zote za mpango wako mpaka upate uhakika kuwa utapata fedha-kuzuia kuibiwa mawazo).


5. Uwekezaji Binafsi (Kuweka Akiba)
Inasemekana kuwa zaidi ya asilimia 50 ya bishara ndogo zonazoanzishwa huanza kutokana na akiba binafsi ya wamiliki.

Mmiliki kupitia nyenzo zilizopo za kupata kipato kama ni kazi au biashara nyingine iliyosimama tayari anaweka akiba maalumu kwajili ya kuanzisha biashara mpya. Kiasi cha kuanza kikifikiwa basi fedha hizo zinaingizwa katika biashara mpya.

Fedha hizi zinaweza zikaingizwa kama mkopo binafsi ambapo baadae zitarudishwa katika akaunti binafsi ya mmiliki au zikaingia kama uwekezaji katika biashara ambapo mmiliki atapata faida tu itakayozalishwa.

Vyovyote vile njia hii ni nzuri kwani hakuna madeni toka nje na unaweza ukawa na amani sana katika uendeshaji wake.

Kama wewe ni mwajiriwa na unafikiria kuwa na bishara yako basi njia hii ya kuweka akiba kwajili ya bishara yako ni njia sahihi.

Unaweza ukafungua akaunti nyingine nje na ile ya kawaida na kuhamisha asilimia fulani kila mwezi kwenda katika akaunti hiyo ya biashara (10-25% ni kiwango kizuri)

Ukitaka Mafanikio Ni Lazima Uchukue Hatua Za Haraka
Imesemwa kuwa usisubiri hadi kila kitu kikamilike ndio uanze,katika biashara hiyo inaweza kuwa ngumu au ikakufanya usianze kabisa.

Kama tayari una mpango wa bishara unaovutia usisite kuanza kwa kukosa mtaji,chagua njia mojawapo ya kupata mtaji na uanze.

Ukitaka kupanda jengo la ghorofa ndefu,anza ngazi ya kwanza na utajikuta uko juu .
Ukisubiri kufanya yote kwa mara moja huenda usifanye kabisa. Unapoanza kufanya kitu unapata urahisi kwa jinsi ambavyo unaenda mbele na njia inakuwa wazi kwako katika kila hatua unayochukua.