Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, March 2, 2017

Wizi wa viatu wampeleka mtu jela

Dar es Salaam. Mahakama ya Wilaya ya Ilala, imewahukumu kifungo cha miaka mitatu jela, wakazi wawili wa jiji hili baada ya kupatikana na hatia ya kuvunja stoo na kuiba katoni 384 za viatu aina ya Rubber vyenye thamani ya Sh 45.3milioni.
Washtakiwa hao ni Feisal Mbago(26) na Hassan Hatibu(26) na wamehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kuridhishwa na ushahidi wa mashahidi watatu.
Pia mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa wa tatu ambaye ni Seleman Hamisi(23) baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha shtaka linalomkabili.

0 comments:

Post a Comment