Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Wednesday, March 15, 2017

Wakazi kuchanga Sh494 milioni kujenga shule

Jumla ya Sh494 milioni zinatarajiwa kukusanywa kwa ajili ya ujenzi wa sekondari ya Kata ya Picha ya Ndege Halmashauri ya Mji Kibaha mkoani Pwani,.
Wakazi wa Mtaa wa Mharakani wakiwamo Diwani wao, Robert Machumbe waliafiki kuchangia kiwango hicho.
Kiwango hicho cha fedha kinatarajiwa kukusanywa kutoka kaya 16,467 za kata hiyo, huku kila moja ikichanga Sh30,000 kila moja.
Machumbe amesema ujenzi wa sekondari hiyo unapaswa kupewe kipaumbele mbali na kuwapo changamoto zingine.
Mkazi wa eneo hilo, Godfrey Mwaipopo amesema ili kufanikisha ujenzi huo kwa wakati, ni vyema ikawekwa mikakati itakayowabana baadhi ya wazazi watakaokwepa kuchangia.

0 comments:

Post a Comment