Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Sunday, March 12, 2017

Waitaliano wamtumia sumu Rais wa Real Madrid

Hispania .Polisi nchini Hispania wameanza kuchunguza tuhuma zilizotolewa na maofisa wa klabu ya Real Madrid kwamba kifurushi kilichotumwa kwa rais wa timu hiyo, Florentino Perez kilikuwa na poda inadhaniwa kuwa ni sumu.
Tukio hilo lilitokea juzi, hata hivyo uongozi wa timu hiyo umetoa taarifa polisi ili lichunguzwe kwa kina.
Taarifa kutoka vyombo vya habari nchini humo zilieleza kwamba, mzigo huo ulitumwa kutoka Italia.
Wiki hii Real Madrid ilikutana na timu ya Napoli ya Italia kwenye mchezo wake wa hatua ya 16 bora mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Madrid iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuiondoa Napoli kwa jumla ya mabao 6-2.
Hadi mapumziko timu hiyo ya Italia ndiyo iliyokuwa ikiongoza kwa 1-0. Hata hivyo mabao ya Madrid yaliwekwa kimiani na Sergio Ramos aliyepiga mawili na Alvaro Morata.

0 comments:

Post a Comment