Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Saturday, March 11, 2017

Vijiji 13 vyavamiwa na wachimbaji madini

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumia Maji Zigi Juu (Uwamaziju) katika Wilaya Handeni mkoani Tanga, Phillip Mdoe amesema vijiji 13 vimevamiwa na wachimbaji wa madini na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akizungumza kwenye mkutano ulioandaliwa na Bodi ya Maji ya Bonde la Pangani, Mdoe amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Ubiri, Sakare, Kwemwewe, Mlesa, Mbomole, Shebu, Maramba, Amani, Mgambo, Kwemsisi, Shambangeda, Misalai na Kidugo.
Amesema uharibifu umekuwa ukifanyika katika maeneo hayo kiasi cha kuathiri shughuli za kawaida za uhifadhi wa vyanzo hivyo.
Akizungumzia hali hiyo ya uharibifu wa mazingira, ofisa wa polisi, Michael Joseph amesema kuna baadhi ya wenyeviti wa Serikali za vijiji vinavyozunguka vyanzo vya maji wanaodaiwa kushirikiana na wachimbaji kuharibu vyanzo hivyo.
Joseph amesema jamii inayozunguka maeneo husika inapaswa kuwabana ili wahakikishe kwamba hakuna uharibifu unaoendelea.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mwanaasha Tumbo ametoa siku saba kwa wenyeviti wa Serikali za vijiji vilivyopo katika Tarafa ya Amani kuwakamata wanaochimba dhahabu kwenye vyanzo vya maji, vinginevyo ataagiza wao wakamatwe.
Tumbo ameamua kutoa amri hiyo baada ya wachimbaji wadogo wa dhahabu kuongezeka katika vyanzo vya maji vilivyopo kwenye milima ya Usambara.

0 comments:

Post a Comment