Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Monday, March 13, 2017

Shule 10 kugawiwa Laptop

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, leo anatarajiwa kuzindua Mpango wa ugawaji wa vishkwambi (Ipad) 5,000 na kompyuta mpakato (laptop) na projector kwa shule 10 zilizopo Manispaa ya Dodoma.
Akizungumza jana kuhusu uzinduzi huo, Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, alisema huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ahadi walizotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kwa wananchi.
Mavunde alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa ufadhili wa nchi ya Hispania kwa kushirikiana na Don Bosco.
“Upatikanaji wa vifaa hivi Ipad vishkwambi utamrahisishia mwanafunzi namna bora ya kujisomea vitu vingi kwa wakati mmoja,”alisema Mavunde.
Alisema wanaendelea kutembea kwenye ahadi zao na si kuishia kwenye maneno badala yake wanafanya utekelezaji.
Mavunde alisema vifaa hivyo vitahifadhiwa shuleni, pia vitawekwa vitabu vya kusomea ambavyo vinakwenda sambamba na mtaala wa elimu ya msingi.
"Kupitia mpango huu wa matumizi ya teknolojia ya kisasa, itasaidia kuwafanya wanafunzi wengi zaidi kushiriki katika kujisomea na hivyo kusaidia kuongeza maarifa zaidi miongoni mwao," alifafanua.
Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Bunge, Sera, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, alisema vifaa hivyo vitakabidhiwa kwa walimu ambao watafika kwenye hafla hiyo kwa ajili ya kuwakilisha shule zao.

0 comments:

Post a Comment