Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Friday, March 10, 2017

Jaji atoa mpya amuuliza aliyebakwa ''kwa nini hakufunga miguu''Canada

Jaji Camp
Jaji wa mahakama ya juu nchini Canada amemuuliza mwathiriwa wa ubakaji kwa nini hakufunga miguu
Jaji mmoja kutoka Canada aliyemuuliza mwanamke katika kesi ya ubakaji ''kwa nini hakuweka mapaja yake pamoja'' wakati wa tukio hilo amejiuzulu.J
Robin Camp alijiuzulu baada ya kamati ya nidhamu kupendekeza kuwa afutwe kazi.
Bwana Camp alisema kuwa alisikitishwa na matamshi yake lakini jopo la nidhamu lilisema liliona matamshi yake yalikosa hali ya kutopendelea na heshima.
Waziri wa haki katika jimbo hilo amekubalia kujiuzulu kwake.
Matamshi ya bwana Camp yaliotolewa wakati wa keshi ya ubakaji mwaka 2014 yalizua hisia kali na kusababisha ukosoaji mkali kutoka kwa waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono pamoja na mawakili wao.Jaji huyo alichukua msimamo na kuliambia baraza hilo kwamba alifahamishwa kuhusu makosa yake na kwamba aliomba msamaha juu ya matamshi yake.
Baraza hilo ambalo husimamia idara ya haki lilibaini kwamba vitendo vya bwana Camp wakati wa keshi hiyo vilikuwa na uharibifu wa wazi kuhusu sera ya kutoa haki katika idara hiyo na kwamba hawezi kuendesha tena afisi hiyo.
Pia ilibainika kwamba jaji huyo alizungumza na mlalamishi kwa lugha isioheshimika inayofedhehesha na kuonyesha ubabe.

0 comments:

Post a Comment