Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Friday, February 24, 2017

Wananchi waukataa mradi Kagera

Wananchi wa Kijiji cha Kyota, mkoani Kagera wameukataa mradi wa umwagiliaji wenye thamani ya Shs. 234.7 milioni uliokamilika tangu Juni 2015 baada ya kupata hasara ya mavuno ya mpunga. - Hasara imetokea baada ya mkandarasi wa mradi kuzima mashine za kusukuma maji mashambani mara tu baada ya mpunga kupandwa akitaka kwanza halmashauri ya wilaya imlipe fedha iliyobaki ili akabidhi mradi. imearifiwa kwamba, hali hiyo ilisabababisha mpunga kunyauka kwa kukosa maji baada ya kuwekwa mitaro inayovuna hata maji ya mvua na kuyapeleka mtoni ili yasukumwe kwa mashine yatakapohitajika mashambani. Wakulima hao wanasema kwamba, kabla ya ujio wa mradi huo na kujengwa kwa miundombinu ya umwagiliaji walivuna magunia 20 hadi 25 ya mpunga kwa ekari moja. “Katika mavuno ya mwaka huu tumepata kati ya gunia 2 hadi 5 kwa ekari moja baada ya mpunga kukauka kwa kukosa maji,” wamesema wakulima hao

0 comments:

Post a Comment