Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Monday, February 20, 2017

Mazungumzo ya kutatua mgogoro wa Burundi umekamililsha awamu ya tatu.

Msuluhishi wa mazungumzo ya kutatua mgogoro wa burundi rais mstaafu wa tanzania Mh. Benjamin Mkapa amekamililsha awamu ya tatu ya mazungumzo ya kutatua mgogoro huo yaliyokuwa yanafanyika jijini Arusha ambayo amesema yamekuwa na ufanisi mkubwa na hatua iliyofikiwa ni nzuri.
Akizungumza wakati anatoa majumuisho ya kikao hicho Mh.Rais Mstaafu mkapa amesema baada ya kukutana na makundi yote na kusikiliza hoja zao sasa anatarajia kukutana na Mwenyekiti wa usuluhishi wa mgogoro huo Rais. Yoweri Mseven na pia mkuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hata hivyo Mh. Mkapa amesema kinahotia moyo ni kuona asilimia kubwa ya wajumbe wa pande zote wanakubaliana na  mapendekezo ya kuhakikisha kuwa suala la utulivu wa kisiasa, ustawi wa kiuchumu , na Mahusiano ya Burundi na nchi zingne yanapewa kipaumbele.
Wakizungumza baada ya kumalizika kwa kikao hicho katibu mkuu wa chama tawala cha (CNDD  -FDD) Bw. Evariste Ndayishimiye, kiongozi wa kundi la Sinared ambao ni wapinzani wakubwa wa serikali Bw,Jean Minan, na baadhi ya wajumbe pamoja na kukiri kuwa hatua iliyofikiwa inaleta matumaini kila mmoja ameendelea kushikilia msimamo wake.
Pamoja na hatua hiyo kubwa iliyofikiwa na msuluhishi wa mazungumzo hayo bado kuna changamoto nyingi ikiwemo ya kundi la Sinared kutokuwa tayari kukaa meza moja na makundi mengine kwa madai kuwa wao wanataka kuonana na serikali ambayo nayo haiko tayari.

0 comments:

Post a Comment