Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, February 23, 2017

Mavugo Aandaliwa kuifunga Yanga Jumamosi,Simba Yampa Uchezaji Bora Wa Januari

KIASI cha siku tatu kabla ya kupambana na mahasimu wa jadi, Yanga – klabu ya Simba imemjenga kisaikolojia mshambuliaji wake, Mrundi Laudit Mavugo kwa kumtangaza Mchezaji Bora wa klabu wa mwezi Janauri. Taarifa ya Simba SC leo imesema kwamba Mavugo ndiye mchezaji bora wa klabu kwa Januari na atapatiwa Sh. 500,000 na taji kwa ushindi huo. Kwa sasa Simba ipo kambini kisiwani Zanzibar ikijiandaa na mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu, Yanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo wa marudiano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, unafuatia ule wa mzunguko wa kwanza, ambao timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Uwanja wa Taifa pia Oktoba 1, mwaka jana. Yanga wao wameweka kambi eneo la Kimbiji, Kigamboni, Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu.

0 comments:

Post a Comment