Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, January 26, 2017

Kanda Bongo Man aomboleza kifo cha baba yake Pam D aliyekuwa mpiga gitaa la base kwenye bendi yake

Muimbaji mashuhuri na mkongwe wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kanda Bongo Man, ameomboleza kifo cha baba yake msanii wa Bongo Flava, Pam D, Shedrack Nyato. Nyato alikuwa mpiga gitaa la base kwenye bendi ya muimbaji huyo na walisafiri pamoja kutumbuiza kwenye nchi mbalimbali. Baba yake Pam D (anayepiga gitaa) akitumbuiza pamoja na bendi ya Kanda Bongo Man Bongo Man amemtumia ujumbe wa WhatsApp Pam D na kumuomba asome maneno aliyoandika kabla hajazikwa. “Hey Festo jamaa yangu, tulisafiri wote Marekani, Canada, Zimbabwe, Visiwa vya Komoro, Mayotte, Reunion Island, Malawi na Australia. Hukuwa tu mwanamuziki bora niliyekutana naye katika maisha yangu lakini mmoja wa wanamuziki niliowachagua kutumbuiza pembeni yangu. Mungu akubariki na lala salama. Ujumbe toka kwa Bongo Man,” ameandika kwenye ujumbe huo.

0 comments:

Post a Comment