Tuesday, December 13, 2016
PAUL MAKONDA azindua ujenzi wa barabara
Mkuu wa Mkoa wa Dsm Paul Makonda amezindua Ujenzi wa barabara ya Kilometa moja itakayogharimu kiasi cha Shilingi Milion 760 itakayojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Grand Tech Ltd baada ya kuitikia wito wa kuisaidia Serikali ya awamu ya tano itakayoanzia Kurasini-bandarini hadi ukanda wa biashara wa EPZ .
Akizungumza mara baada ya Uzinduzi huo Makonda amesema kampuni hiyo imeonyesha Uzalendo katika kuisaidia serikali ya Mkoa wa dsm ambapo itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha Zege au Conglete kutokana na eneo hilo kutumika na magari makubwa yanayoingia bandarini kuchukua mizigo na makontena.
Amesema bado katika baadhi ya barabara katika jiji la dsm ziko katika hali mbaya na kuwataka wadau mbali mbali wa maendeleo kujitokeza ili kupunguza changamoto ya barabara mbovu licha ya serikali ya Mkoa kutafuta suluhisho la kudumu katika ujenzi wa barabara katika jiji la Dsm.
Katibu tawala wa manispaa ya Temeke Hashim komba amesema Ujenzi huo utasaidia kuboresha ukanda huo wa bandarini ambao serikali imeutenga kwa ajili ya Shughuli za Bandari,kuhusu baadhi ya wananchi wenye nyumba 12 ambazo zinatakiwa kuvunjwa ili kupisha Ujenzi huo amesema tayari suala lao limefikia katika hatua nzuri .
0 comments:
Post a Comment