Ujenzi
wa barabara ya kuanzia Tengeru Arusha hadi Taveta Voi ya ukubwa wa km
234.3 iliyozinduliwa March 3 mwaka huu na Rais John Magufuli, wakati
ujenzi ukiendelea kumetokea ajali ambapo Raia wa china Eng. Pil soo shin
amekandamizwa na mtambo wa kushindilia lami na kufariki dunia.
Kwa
mujibu wa balozi wa eneo la kwa mrefu ambaye pia ni shuhuda amesema
marehemu alikuwa akisimamia zoezi la kushindilia lami kwenye barabara na
mwendesha mtambo hakumuona, jambo lililopelekea suruali yake kushikwa
na nondo iliyokuwa karibu hivyo akaangukia barabarani na mtambo
ukamkanyaga.
Jeshi
la polisi kupitia kwa kaimu kamanda wa polisi Arusha Yusuph Ilembo
amesema kwamba mtuhumiwa aliyesababisha kifo hicho kwa uzembe bado
anashikiliwa na polisi na uchunguzi ukikamilika atapelekwa mahakamani
0 comments:
Post a Comment