Kutoa mimba ni nini? Hii ni hali ya mwanamke kwa hiari yake mwenyewe kuharibu mimba iliyoingia ndani ya kizazi chake.
Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za 
uzazi wa mpango kwa watu wengi walioko kwenye mahusiano, wasichana wengi
 kwa sasa wanatoa mimba.
Utafiti nilioufanya mwenyewe nimegundua kwamba zaidi ya asilimia tisini 
ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja 
kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua 
kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano.
 Sasa unajiuliza bado kuna mtu humo au mfu?
Hata hivyo hao wanaozaa pia hujikuta wamebeba mimba zingine wakati 
watoto wao wakiwa wadogo na kulazimika kuzitoa. Najua watu wengi wanatoa
 mimba kukwepa aibu, kutokua tayari kisaikolojia na kadhalika lakini ni 
bora kutumia njia za uzazi wa mpango kama condomu kuzuia mimba na kama 
kondomu huiwezi basi tumia njia zingine kama sindano na vijiti kwasababu
 wengi wenu mkishalewa pombe au kondomu isipokuepo ndio basi tena.
Hebu tuyaangalie madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…
Uwezekano mkubwa wa kufa:
Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba 
wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano wa kufa mara nne zaidi kuliko 
ambao hawatoi mimba. Vifo hivyo vimekua vikisababishwa na kujiua wenyewe
 kutokana na kujuta kwa maamuzi yao na madhara ya mda mrefu ya kimwili 
yatokanayo na kutoa mimba. Vifo ndani ya wiki moja baada ya kutoa mimba 
hutokana na kuvuja damu sana, madhara ya dawa za usingizi, mabonge ya 
damu kwenye mishipa ya damu na mimba iliyotunga nje ya uzazi. Utafiti 
pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili
 114%, mimba tatu 192%.
Ugumba kwa wanawake wengi:
Miaka hii ya karibuni wanawake wengi ambao wanalia kutopata watoto wana 
historia za kutoa mimba miaka iliyopita, na wengi wao nilionana nao 
wanajuta sana kwa maamuzi yao. Hii inatokana na madhara makubwa 
waliyoyapata kwenye mfuko wa uzazi baada ya mimba kutoka.
Mimba kutunga nje ya kizazi:
Mfuko wa uzazi una utando maalumu amaboa hufanya mimba iliyotungwa 
kwenye mirija iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko
 ya uzazi. Lakini utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo 
na kupoteza utando huo na kusababisha mimba kukulia huko.matibabu ya 
tatizo hili ni kukata mrija husika tu hivyo kuongeza hatari ya ugumba..
Kuzaa watoto wasio na akili nzuri:
Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi kushindwa kushika vizuri 
na matokeo yake mwanamke huyu hujikuta akizaa kabla ya mda husika 
akibeba mimba nyingine. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda
 maalumu  na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua 
wagonjwa wa akili maisha yao yote.
kansa ya mlango wa uzazi
Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa ya kupata kansa ya mlango wa 
uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwasababu ya 
kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa 
mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.
Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku 
za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana 
deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. 
Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati 
hayupo, kua na hasira sana…
Mwisho
kumbuka kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimba...maumivu ya 
kukosa mtoto ni makali sana kuliko aibu ya kuzaa nje ya ndoa. Hawa 
wanaozaa sasa hivi unawaona malaya ipo siku utawakumbuka utakapo ambiwa 
na daktari kwamba labda itokee miujiza ndo utazaa.Kama hutaki mimba 
tumia njia za uzazi wa mpango kwani kuendelea kutoa mimba kutakupa 
adhabu ya kukosa mtoto ambayo adhabu hiyo utaitumikia maisha yako 
yote..kwa maelezo zaidi







 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment