Friday, January 6, 2017
Wananchi wamshinikiza mkuu wa wilaya kuvunja uongozi
Wananchi wa kijiji na kata ya Rwamgasa Wilayani Geita wamemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Herman Kapufi kuvunja uongozi wa kijiji hicho baada ya mkaguzi wa ndani kubaini zaidi ya Shs. Milioni 50 zilitumika bila kuzingatia utaratibu wa Serikali.
Akisoma ripoti ya ukaguzi huo kwenye mkutano wa hadhara mbele ya mkuu wa Wilaya hiyo uliofanyika kwenye uwanja wa kituo cha polisi Rwamgasa uliokuwa na lengo la kuchangia maendeleo na kusiliza kero za wananchi, Mkaguzi wa ndani wa Halimashauri ya Wilaya ya Geita Chacha Masebo amesema fedha hizo zilitokana na makusanyo ya ndani kwenye kijiji hicho.
Mara baada ya mkaguzi huyo kusoma ripoti hiyo wananchi nao wakatoa kero zao mbele ya mkuu wa wilaya hiyo bwana Herman Kapufi.
Baada ya kuwasikiliza wananchi hao, Mkuu wa wilaya hiyo akatoa tamko la serikali.



0 comments:
Post a Comment