Friday, January 6, 2017
Watumishi wanne wafikuzwa kazi mbeya
Halmashari ya Wilaya ya Mbeya imewafukuza kazi watumishi wanne ambao ni wakuu wa idara kwa tuhuma za kufanya uzembe kazini na kuisababishia hasara ya takribani shilingi bilioni moja na nusu.
Image
Sehemu ya Jiji la Mbeya
Uamuzi huo umetangazwa na Mwenyekiti wa halmashauri ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Inyala, Mwalingo Kisemba ambaye amewataja watumishi hao.
Mkurugenzi wa Halmashauri, Americhiory Biyengo amesema yeye kama mshauri Mkuu wa Baraza la Madiwani ametoa ushauri wa kitaalam kuzuia watumishi hao wasifukuzwe kazi, lakini ushauri wake haukuzingatiwa na sasa imembidi kutekeleza uamuzi wa Baraza la Madiwani.
Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa watumishi hao wanayo nafasi ya kukata rufaa kwenye mamlaka za juu zaidi, na kudai kuwa endapo uamuzi wa kuwafukuza kazi utatenguliwa, Halmashauri hiyo inaweza kupata hasara kubwa ya kuwalipa fidia.



0 comments:
Post a Comment