Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, March 16, 2017

Zanzibar yatambuliwa rasmi CAF

Shirikisho la soka Afrika (Caf) limeridhia kuipa uanachama wa kudumu Zanzibar kuanzia leo.
Ombi hilo limeridhiwa na mkutano mkuu wa Caf unaondelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
"Ombi la Zanzibar limepita bila kuwekewa pingamizi. Zanzibar sasa ni mwanachama wa 55 wa Caf, " uliandika ukurasa wa Twitter wa shirikisho hilo.
Kwa kupata nafasi hiyo, no rasmi sasa timu ya taifa na Zanzibar itapata fursa ya kushiriki mashindano yote yanayoandaliwa na Caf.
Zanzibar sasa itaweza kushiriki mashindano yanayoandaliwa na CAF kama vile Mataifa ya Afrika (AFCON), fainali za Afrika Wanawake (AWCON), fainali za vijana (AFCON U17 na AFCON 20).
Pia, itakuwa na uhalali wa kuhudhuria mikutano mbalimbali sanjari na kupokea na kusimamia kozi mbalimbali na kupata fursa ya ya kupiga kura katika masuala muhimu ya CAF.
Hivi sasa Zanzibar inapata fursa ya klabu zake zinazoshika nafasi ya juu katika Ligi Kuu ya Zanzibar kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.

0 comments:

Post a Comment