Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Saturday, March 4, 2017

Wanajeshi Wanywa Damu ya Cobra Kambini ili kuweza kukabiliana na wanyama porini

Wanajeshi wa Kimarekani zaidi ya 3000, wapo katika mafunzo ya kijeshi huko Sattahip, Thailand yanayohusisha kunywa damu ya nyoka aina ya Cobra na kumchinja kuku hai kwa mdomo.
Wanajeshi hao wa jeshi la Wanamaji na mabaharia walioshiriki mafunzo ya siku kumi walifanya jaribio la kukata kichwa cha kuku mzima kwa mdomo na wanyama wengine jamii ya reptilia.
Kiongozi wa Jeshi la Wanamaji, Harry B. Harris alisema katika taarifa yake kuwa mafunzo hayo yanajumuisha namna ya kukabiliana na wanyama wa porini, kujihami na wanyama mazoezi makali ya moto.
“Kunywa damu ya cobra ni sehemu ya mafunzo ya kukabiliana na mazingira ya porini.” alisema Harris
Pamoja na Marekani, nchi nyingine zilizoshiriki katika mafunzo hayo makali ni Thailand, Singapore, Japana, Indonesia na Malaysia.

0 comments:

Post a Comment