Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Tuesday, March 14, 2017

Serikali yawahakikishia wananchi vijijini kupata umeme wa uhakika kupitia miradi ya REA ya awamu ya tatu

Shirika la maendeleo ya petrol nchini TPDC katika kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya mafuta na gesi limeanza kutoa mafunzo kwa walimu wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari za Lindi na Mtwara ili kuwajengea uwezo wa kuwafundisha wanafunzi wanaopenda masomo ya sayansi.
Shirika hilo limefungua klabu mbalimbali za wanafunzi katika shule za sekondari katika mikoa ya lindi na Mtwara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi kuielewa sekta ya mafuta na gesi.
Kwa kutambua hilo walimu wa masomo ya sayansi wanapewa mafunzo yanayohusu sekta ya mafuta na gesi ili waweze kuwafundisha wanafaunzi kupitia klabu walizounda ili kufanya wanafunzi kupenda masomo hayo.
Licha ya mafunzo hayo kutolewa walimu wanadai kuwa dhana za kufundishia bado ni tatizo katika kufikia lengo la kuwa na wataalamu wa mafuta na gesi watokanao na klabu zilizoundwa.

0 comments:

Post a Comment