Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Saturday, March 18, 2017

Ridhiwani Kikwete Afunguka Ya Moyoni Kuhusu Dawa Za Kulevya

Dar es Salaam. Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete amesema Serikali haina budi kuweka msimamo kuhusu chombo cha kushughulikia vita dhidi ya dawa za kulevya badala ya hali iliyopo sasa inayozua minong’ono.
Aliyasema hayo jana alipozungumza na Radio Uhuru ikiwa ni siku moja baada ya kuhojiwa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.
Ridhiwan aliitwa na Kamishna Sianga kuhojiwa kuhusu biashara na matumizi ya dawa za kulevya, ikiwa ni sehemu ya vita inayoendelea nchini ya kukabiliana na dawa hizo haramu.
Akizungumza na Radio hiyo, Ridhiwan alisema hadi sasa haieleweki ni chombo gani hasa kinachoongoza vita hiyo.
“Kwa Sianga unahojiwa na kuelezwa matokeo ya mahojiano, kwa Mzee (kamanda wa Polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon) Sirro unakamatwa, unatangazwa, unaaibishwa,” alisema Ridhiwan.
Alisema hali hiyo inakanganya watu kwa kuwa vyombo hivyo viwili vinatumia mbinu tofauti.
“Mimi niliitwa kuhojiwa na baadaye kuachiwa. Wengine wanakamatwa na Mzee Sirro na kuwekwa mahabusu. Kama akina Vanessa Mdee, wameshikiliwa huko na sijui hata kama wameshaachiwa,” alisema Ridhiwani.

0 comments:

Post a Comment