Danielle van de Donk alifungia Arsenal mabao mechi 20 msimu uliopita
Mabingwa watetezi wa Kombe la FA Uingereza upande wa wawanawake Kina dada wa Arsenal waliwalaza wapinzani wao Tottenham 10-0 na kufika robo fainali Jumapili.
Danielle van de Donk alifungia wenyeji hao mabao matatu, naye mshambuliaji wa zamani wa Sunderland Beth Mead akafunga bao pia mechi yake ya kwanza kuchezea Arsenal.
Chelsea, ambao walishindwa na Arsenal fainali mwaka jana, pia walipata ushindi mkubwa, kwa kulaza Doncaster 7-0.
Bristol City walilaza Millwall 5-0.
Liverpool, Notts County, Birmingham na Sunderland pia walishinda kwenye mechi hizo za raundi ya tano.
Droo ya robofainali itafanyika baadaye Jumatatu.
Matokeo kamili mechi za raundi ya tano
Manchester City 1-0 Reading (Jumamosi)
Arsenal 10-0 Tottenham
Birmingham 2-0 West Brom
Bristol City 5-0 Millwall
Chelsea 7-0 Doncaster
Liverpool 2-1 (AET) Everton
Notts County 3-2 Yeovil
Sunderland 3-2 Aston Villa
Monday, March 20, 2017
Kina dada wa Arsenal walaza Tottenham 10-0
By EPAMA2255 HABARI at 3:29 AM
No comments
0 comments:
Post a Comment