Thursday, February 16, 2017
Serikali kununua Rada nne kuwezesha kuona aina yoyote ya ndege inayoingia ama kupita katika anga la Tanzania
Serikali imesema itanunua rada nne ambazo zitawekwa sehemu mbali mbali za Tanzania ili kuwezesha kuona aina yoyote ya ndege inayoingia ama kupita katika anga la Tanzania ili kuhakikisha nchi ya Tanzania inakuwa salama mda wote.
Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mtwara waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Professor Makae Mbalawa ambae ametembelea uwanja wa Ndege,kivuko cha mpakani mwa Tanzania na msumbiji cha Mvi Kilambo pamoja na bandari,amesema kuwa kwa sasa serikali imefikia uamuzi huo wa kununua rada nne kwa kuwa kuna maeneo mengine hayaonekani katika rada iliyopo.
Aidha rada hizo zitasaidia kuona ndege ndogo ndogo ambazo zinatua katika migodi ya madini ambazo hazijulikani zinabeba nini.
0 comments:
Post a Comment