Thursday, February 16, 2017
Hatma ya Wenger kujulikana mwisho wa msimu
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger baada ya timu yake kula kichapo cha bao 5-1 na Bayern Munich
Uamuzi kuhusu hatma ya mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger utafanywa mwisho wa msimu huu lakini kandarasi mpya inamsubiri kwa sasa.
Licha ya kichapo cha siku ya Jumatano katika uwanja wa Bayern Munich hakuna mpango wa Wenger kuondoka baada ya msimu huu.
Inaaminika kwamba uamuzi wa yeye kusalia ama kuondoka utaafikiwa kati ya klabu hiyo na raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 67.
Wenger ambaye amekuwa akisimamia timu hiyo tangu 1996 alipewa kandarasi mpya mapema msimu huu.
Yeye hutoa uamuzi wake baada ya mwisho wa msimu wakati anapoangazia matokeo ya timu hiyo na kile kinachopaswa kufanywa siku za usoni.
Kandarasi yake na klabu hiyo ya Uingereza inakamilika mwishoni mwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment