Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Tuesday, February 14, 2017

Mwanaridha Nade afungwa chuma mguuni

Arusha. Mwanariadha chipukizi Kalisti Nade aliyevunjika mguu baada ya kugongwa na pikipiki mazoezini huko Manyara amefungwa vyuma katika mguu wake. Nade alikuwa akijiandaa na Mashindano wiki hii mkoani Kilimanjaro yenye lengo la kupata timu ya Taifa kwa ajili ya mashindano ya Mbio za Nyika yatayofanyika Uganda mwezi ujao. “Ninamshukuru Mungu baada ya upasuaji wiki iliyopita, kwa sasa ninaendelea vizuri japo daktari amenishauri niendelee kubaki hospitali kwa uangalizi wa karibu,” alisema Nade. Chipukizi huyo alisema tatizo linalomkabili ni ukosefu wa fedha za matibabu japo anashukuru Kituo cha Shahanga Sports Institute kilinachomilikiwa na mwanariadha mkongwe Gidamis Shahanga huko Katesh kwa kumsaidia. “Kweli ndoto zangu zimekatishwa maana familia ilikua inanitegemea kwa kile kidogo ninachokipata kwenye mashindano na kwa sasa daktari ameniambia nisifanye lolote kwa muda wa mwaka mmoja ila kila mara niwe naenda kuchunguzwa,” alisema Nade. Mwanariadha huyo akiwa kwenye moja ya ratiba yao kwenye mazoezi pamoja na wenzake alijikuta akiparamiwa na pikipiki iliyomshinda dereva na kumsababishia majeraha. “Ni pigo kubwa kwa kituo chetu kwa kuwa ni mwanariadha aliyekuwa akija juu katika tasnia hii.” alisema Shahanga.

0 comments:

Post a Comment