Tuesday, January 31, 2017
Zaidi ya wanafunzi 3685 Sikonge Tabora hawajui kusoma,kuandika na Kuhesabu
Zaidi ya wanafunzi elfu tatu mia sita themanini na tano katika shule za msingi za wilaya ya Sikonge mkoani Tabora hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu ikiwa ni sawa na asilimia 9.7 ya wanafuzni wote wa darasa la kwanza hadi la saba wilayani humo.
Uchunguzi uliofanywa na channel ten umebaini sababu zinazosababisha ni pamoja na Utoro, mimba za utotoni na shughuli za kilimo.
Katika uchunguzi huu Channel ten imefanikiwa kuzungumza na baadhi ya walimu wa shule za msingi wilayani humu..
HILALI BITWAYE ni Afisa elimu wa shule za msingi wilayani sikonge anatoa msimamo wa kuhakikisha wanafunzi wanajua kusoma, kuandika na kuhesabu.
Kwa kuliona hili AGGREY MWANRY ambaye ni mkuu wa mkoa wa TABORA anaeleza msimamo wa mkoa.
Mbinu mbali mbali za ufundishaji ni muhimu kwa watoto hawa.




0 comments:
Post a Comment