Tuesday, January 31, 2017
NECTA wamesema Ufaulu wa masomo haya bado upo chini ya Asilimia 50
Baraza la mitihani Tanzania – NECTA limetangaza matokeo ya kidato cha nne na maarifa uliofanyika novemba mwaka 2016 ambapo kiwango cha ufaulu kimeonekana kuongezeka kwa asilimia 2.44 kutoka asilimia 67.91 mwaka 2015 hadi 70.35 mwaka 2016 huku mkoa wa Dar es salaam ukishika nafasi za mwisho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu mtendaji NECTA Dk.Charles Msonde amesema Licha ya ufaulu wa jumla kuendelea kuimarika takwimu zinaonesha kuwa bado ufaulu wa masomo ya civics, history, physics,basic mathematics, commerce na book-keeping upo chini ya asilimia 50 huku idadi ya waliofaulu vizuri kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ikiwa asilimia 27.60 ya watahiniwa wote waliofanya mtihani huo.
Dk.Msonde amezitaja shule zilizofanya vizuri zikiongozwa na feza ya wavulana Dsm,St.Francis Mbeya nafasi ya tatu ikishikwa na kaizirege juniour ya Kagera huku shule kumi za mwisho, sita zinatoka mkoa wa Dsm ikiwemo shule ya Kitonga na Nyeburu.
Vyombo vya habari vilipata fursa ya kuzungumza na mwanafunzi aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa Alfred Shauri pamoja na mkurugenzi wa shule za Feza Tanzania Ibrahim Rashid.
Kwa Mujibu wa NECTA watahiniwa 126 wamefutiwa matokeo yao kutokana na kubainika kufanya vitendo vya udanganyifu ambapo mmoja kati ya hao aliandika matusi katika karatasi yake ya majibu.




0 comments:
Post a Comment