Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Saturday, January 28, 2017

Nguvu yatumika kuwaondoa wafanya Biashara Morogoro

PICHA: Nguvu yatumika kuwaondoa wafanya Biashara Morogoro Saturday, January 28, 2017 Jeshi la polisi wakishirikiana na mgambo wa Manispaa ya Morogoro wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyabiashara wadogo wanaopanga bidhaa kando ya barabara katikati ya mji huku wafanyabiashara wadogo katika soko la nanenane wakiugulia maumivu baada ya halmashauri hiyo kuvunja meza zao walizo jenga nje ya soko na kuwataka waondoka maramoja waende katika maeneo waliyopangiwa. Operesheni ya kuvunja meza na vibanda vya wafanyabiashara waliokaidi amri ya kuwataka kuonoka katika maeneo hayo kwa hiyari imeanza kufanyika majira ya alfajiri katika soko la nanenane ikihusisha mgambo wa manispaa hiyo pamoja na Jeshi la polisi na badaye zoezi kuhamia katikati ya mji. Diwani wa kata ya Tungi Juma Tembo anayelaumiwa na wananchi kuwa aliwambia wafanyabiashara wa nanenane wafanye biashara katika eneo hilo ametupia lawama Mkurugenzi wa manispaa kwa kuchukua uamuzi wa kuwavunjia wafanyabiashara hao. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro John Mgalula amesema wafanyabiashara hao wamekiuka agizo la kuwataka waondoke kwa hiari nakwamba wamenukuu vibaya agizo la Mheshimiwa Rais dakta John Pombe Magufuli.

0 comments:

Post a Comment