Saturday, January 28, 2017
Matonya kuongea tena na Lady Jay Dee
Msanii mkongwe wa muziki Matonya amewaahidi mashabiki wa muziki wake kumtafuta muimbaji Lady Jay Dee ili kuangalia kama wanaweza kufanya remix ya wimbo ‘Anita’ ambao ulifanya vizuri kwa miaka iliyopita.
Amesema hayo Matonya wakati akizungumza live kupitia mtandao wa Instagrma, ambapo alidai ni jambo ambalo linawezekana kwa upande wake.
“Remix ya Anita inawezekana lakini ngoja nimtafute Lady Jay Dee halafu tuangalie kama tunaweza kufanya,” Matonya alimjibu mmoja kati ya mashabiki hao waliouliza kuhusu remix hiyo.
Image result for lady jaydee
Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Hakijaeleweka’.




0 comments:
Post a Comment