Thursday, December 8, 2016
Waziri mkuu ameuagiza uongozi wa hifadhi ya ngorangora kufanya sensa!
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kufanya sensa ya wenyeji wanoishi ndani ya hifadhi hiyo na kuweka alama kwenye mifugo yote ya wenyeji ili kuondoa matatizo yanayojitokeza ndani ya hifadhi hiyo.
Waziri mkuu ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na wafanyakazi na baraza la wafugaji la mamlaka ya ngorongoro baada ya kupokea taarifa ya mamlaka kutoka kwa mhifadhi mkuu Daktari Fred Manongi.
Akisoma taarifa ya mamlaka hiyo kwa waziri mkuu daktari Manongi amesema uongozi umekuwa ukipokea malalamiko mengi kutoka kwa wageni wanatembelea hifadhi hiyo ambao amesema wamekuwa hawafurahishwi na idadi kubwa ya mifugo,magari ndani ya kreta pamoja na makazi ya watu ndini ya hifadhi.
Baada ya kusikia hoja hoyo kutoka kwa mhifadhi mkuu waziri mkuu akatoa agizo hilo ambalo amesema sensa hiyo itasaidia kupanga mipango ya maendeleo kwa wakazi hao baada ya kujua idadi ya wenyeji lakini pia itasaidia kujua fedha zinazotolewa kwa ajili ya baraza la wafugaji zinatumikaje lakini pia kudhibiti wahamiaji haramu na mifugo yao.



0 comments:
Post a Comment