Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, December 8, 2016

JPM AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA SUDANI KUSINI!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Nyandeng Garang de Mabior sambamba na ujumbe wake akiwemo Mabior Garang ambaye ni mtoto wa Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha za Mabior Garang zilizowahi kuzua utata mitandaoni. Mabior Garang aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Sudan Kusini aliwahi kutikisa mitandani kwa picha zake zilizozua utata huku akidaiwa kufukuzwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri na Rais wa nchi hiyo Salva Kiir kwa kile kilichosemwa kuvaa mavazi yasiyostahili. Baaada ya mazungumzo hayo, Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini. Amemuomba Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wajumuia ya Afrika ya Mashariki kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.

0 comments:

Post a Comment