Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Thursday, November 17, 2016

RAIS MAGUFULI ATIA SAINI SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI YA MWAKA 2016

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, inawataarifu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametia saini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 iliyopitishwa na Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wake wa 5 Mjini Dodoma. Rais Magufuli amesaini Sheria hiyo tarehe 16 Novemba, 2016. Dkt. Magufuli amewapongeza wadau wote kwa kufanikisha kutungwa kwa Sheria hiyo. "Naamini kuwa Sheria hii itasaidia kuboresha sekta ya habari kwa manufaa ya wanataaluma wenyewe na Taifa" amesema Rais Magufuli. Gerson Msigwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Dar es Salaam 17 Novemba, 2016

0 comments:

Post a Comment