Tuesday, November 15, 2016
Jela maisha kwa kulawiti
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Mlele moani Katavi, imemhukumu mkazi wa kijiji cha Ilunde, Festo Joseph (29), kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kumlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka tisa.
Hakimu wa mahakama hiyo, Theotimus Swai, alitoa adhabu hiyo jana baada ya mshitakiwa kukiri mahakamani hapo kuwa ni kweli alimtendea unyama huo binti wa jirani yake.
Hakimu Swai alisema licha ya mshitakiwa kuwa amekiri kosa, amelazimika kutoa adhabu hiyo ili iwe fundisho si kwake tu, bali kwa wengine wenye tabia kama zake.
Awali, Mwendesha Mashitaka, Baraka Hongoli, alidai kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo saa 9:00 alasiri ya Novemba 10, mwaka huu, kijijini Ilunde.
Alidai mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mshtakiwa alifika nyumbani kwa wazazi wa mtoto huyo ambapo alimdanganya kuwa baba yake ambaye hakuwepo nyumbani hapo, alimtuma akamuoneshe nyasi alizokata kwa ajili ya kuezekea nyumba yao.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka huyo, mshtakiwa aliongozana na mtoto huyo hadi porini ambako alimlawiti.




0 comments:
Post a Comment