Wednesday, October 19, 2016
Moto wateketeza Mabweni 2 ya Shule ya Kondoa Islamic
Moto wateketeza Mabweni mawili ya wasichana ya Shule ya Sekondari ya Kondoa Islamic iliyopo Kondoa Mjini, Moto huo ulianza majira ya saa 3 usiku kuamkia leo na kusababisha taharuku kubwa kwa wanafunzi na wazazi kwa ujumla ndipo juhudi za kuuzima Moto huo zikaanza na kuweza kuafanikiwa kuuzima moto huo majira ya saa 5 usiku.
Hata hivyo kamati ya ulinzi na salama ya Wilaya ilifika hapo shuleni na kujionea uharibifu huo, mpaka sasa haijafahamika chanzo cha Moto huo na hasara kwa ujumla.



0 comments:
Post a Comment