Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Sunday, June 4, 2017

Jinsi ya kununua domain

PART 1: JINSI YA KUNUNUA DOMAIN NA KUIWEKA KWENYE BLOG YAKO | FROM .BLOGSPOT TO .COM

Slaus Technologies Tz1 / 5 days ago

Habari za wakati huu msomaji wa Blog yako pendwa ya Slaus Technologies Tz1! Katika mfululizo wa makala za wiki hii, leo tutaangalia jinsi ya kununua domain yako ya .com na kuiweka kwenye blog yako ya .blogspot. (ONLY FOR BLOGGER TODAY).


Image by Slaus Technologies Library
MAHITAJI MUHIMU

1. Lazima uwe na kadi ya benki yenye uwezo wa kufanya malipo online, eg. MasterCard, VISA, etc! au PayPal.

2. Uwe na blog ya blogger, eg slaustectz1.blogspot.com, kama bado ingia blogger.com

3. Umakini kidogo.

FAIDA ZA NJIA HII

**Hautapoteza wasomaji wako waliokuwa wanatumia blog yako ya.blogspot kwa sababu watapelekwa moja kwa moja kwenye hio domain yako utakayonunua. Kuhakikisha hili, ingia slaustectz1.blogspot.comkuona itakapokupeleka.>>***

HATUA KWA HATUA

Kwa leo nitaelekeza kwa kutumia GODADY, sehemu ambapo huwa napenda kuwanunulia wateja wangu domain names na kuwafanyia setting! Kwa hio kama utakuwa unahitaji kuelekezwa kwa site nyingine utatoa maoni yako na tutayafanyia kazi!

1. Ingia godady.com, create account na nenda moja kwa moja sehemu ya kusearch domain na andika domain unayoitaka ili kuona kama imeshatumika au la. Ingiza domain yako, mf slaustechnologies.com halafu click SEARCH!


Image by Slaus Technologies Library

2. Yatatokea majina mengi ambayo hayajatumika, kama inavyoonekana hapa chini kwenye picha. Unaweza ukachukua domain yoyote, sio lazima ya .com, unaweza ukachukua ya .org, .uk etc. Cheki picha hapa chini. Ukishachagua na ikaonekana Your domain is available we click Continue to Cart ili kufuata taratibu zingine za MANUNUZI! 


Image by Slaus Technologies Library

3. Kwenye page itakayofuata achana na huduma wanazokuambia mfano Free Monthly Website, privacy protection etc, we weka NO au ondoa tiki kwenye hizo huduma, then shuka mpaka chini click Continue to Cart with these Options.


Image by Slaus Technologies Library

4. Kwenye page itakayofuata chagua unataka ulipie kwa miaka mingapi, chini ya neno TERM. Kumbuka unaweza ukatumia coupon ambazo zitapunguza gharama yako ya kununua domain. Click hapa kupata coupon, halafu kuiweka kwenye Godaddy clik sehemu imeandkwa Have promotional code. Click +Add halafu Apply. Halafu clik Proceed to Chekout.


Image by Slaus Technologies Library

5. Kwenye page itakayofuata jaza taarifa zako za muhimu, kama jina etc, kwa chini kwenye Payment Information chagua unayotaka wewe, halafu click PLACE YOUR ORDER. Itatokea page ya kushukuru ambayo itaonyesha na risiti ya malipo! 

Image by Slaus Technologies Library

Image by Slaus Technologies Library


MPAKA HAPO UTAKUA UMEKAMILISHA PART 1 YA KUNUNUA DOMAIN. SASA KWENYE SOMO LITAKALOFUATA NITAKUONYESHA JINSI YA KUIUNGANISHA hii Domain na Blog yako ya .blogspot

Kuwa karibu kupata masomo makali kama haya kwa kudownload App yetu kutoka playstore  HAPA!!

Pia usisahau kulike ukurasa wetu wa Facebook kwa kuclik HAPA ili upate kila kinachotokea hapa.





Visit website

0 comments:

Post a Comment