Propela

aa

million ads

Millionaire  Ads

Wednesday, October 19, 2016

mkopo wa elimu ya juu

FOLLOW OFFICIAL MASWAYETU BLOG INSTAGRAM NOW ,KUPATA HABARI KILA SEKUNDE ZINAPOTOKEA BONYEZA HAPA FOLLOW Mikopo bilioni 80/- elimu ya juu yapelekwa vyuoni kwa ajili ya first years 2016/2017 Paun Jotia 09:13:00 No comments [​IMG] Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufund, Stella Manyanya.​ SERIKALI imetoa Sh bilioni 80 kwa ajili ya malipo ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaoanza na wanaoendelea na masomo na wameanza kulipwa jana. Aidha, imewataka wakuu wa vyuo ambao hawajawasilisha matokeo ya wanafunzi wao wanaoendelea na masomo kufanya hivyo haraka ili wakamilishe uchakataji wa mgawo wa mikopo. Katika mwaka huu wa fedha, serikali imetenga Sh bilioni 427 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Stella Manyanya alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akielezea mchakato wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu na kueleza kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya wanaoanza na wanaoendelea katika robo mwaka. Manyanya alisema serikali imetoa fedha zinazotakiwa kukamilisha mchakato wa malipo unaofanyika kuanzia jana baada ya kumalizika kwa uchambuzi kulingana na vigezo. Alisema kwa mujibu wa ulipaji mikopo, inazingatiwa vigezo vya kisheria vya kutoa mikopo kulingana na uhitaji kwa kuangalia anayepewa, kweli ana uhitaji na siyo kwa kila mtu kwani lengo la serikali kusaidia na siyo kuondoa majukumu ya mzazi. Alisema pia wanaangalia bajeti iliyopo kwa wakati huo, kwani kwa mujibu wa Sera ya Elimu ya Mwaka 2014 na matamko ya Rais John Magufuli amedhamiria kuendelea kutoa mikopo kwa wahitaji wote pamoja na kuboresha elimu kwa namna mbalimbali. Alitaja baadhi ya miradi iliyotekelezwa sambamba na kutoa mikopo ni ukamilishaji wa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Mloganzila kwa Sh bilioni 100 pamoja na kukamilisha ukarabati wa vyuo vya ualimu ambapo tayari vyuo 10 vimekamilika. Alisema pia baada ya Rais kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na kuona adha ya wanafunzi kukabiliwa na kukaa mbali na chuo, Sh bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa mabweni 20 katika ghorofa tatu zitakazochukua wanafunzi 3,800. Manyanya alisema pia serikali imelipia ada moja kwa moja vyuoni kwa wanufaika wa mikopo ya Sh bilioni 40 katika vyuo vya serikali na binafsi nchini. Aliwataka wanafunzi wanaolalamika kutopata mikopo kukamilisha kupeleka viambatanisho vyote stahili huku wakihakikisha wanakuwa na vigezo vya ufaulu kwani sasa ufaulu umepanda wengi wamepata daraja la kwanza na pili, hivyo kuchukua hao kwanza na wale wa daraja la tatu wachache. Naibu Waziri alisema kwa yatima wapo wasiopewa mikopo baada ya uchambuzi kubaini kuwa na uwezo wa kujilipia kutoka kwa ndugu au mali zilizoachwa na wazazi hivyo kuna utofauti wa yatima, kwani wapo wahitaji na wasio wahitaji. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Abdul Razaq Badru alisema bodi hiyo hutoa mikopo kwa kuzingatia kozi za vipaumbele kama udaktari au uhandisi kwa ajili ya ujenzi wa wataalamu katika Tanzania ya viwanda. Alisema pia mikopo hutolewa kwa ulinganifu wa uhitaji kwa asilimia huku wakifanya uchambuzi wa kina ili kuwafikia wahitaji wengi na wanufaika kuongezeka kama anavyotaka rais. Katika hatua nyingine, Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu (Tahliso) imesema kuwa muongozo mpya wa utoaji mikopo uliotolewa kwa mwaka huu wa masomo 2016/17 utawahusu wadahiliwa wapya tu wanaoanza masomo. Taarifa iliyotolewa jana na Tahliso kwenda kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu, ilieleza kuwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo ambao wanaendelea na masomo, wao wataendelea na utaratibu kama ulivyokuwa tangu awali walivyoingia makubaliano na utaratibu mpya hautawaathiri. Mwenyekiti wa Tahliso, Stanslaus Kadugalize ambaye amesaini taarifa hiyo, alifafanua kuwa msimamo huo umetolewa baada ya jumuiya hiyo kuingilia kati baada ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kutoa mwongozo wa utoaji mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Kadugalize alisema baada ya kutolewa kwa mwongozo huo walienda kufanya majadiliano na Waziri, Profesa Joyce Ndalichako ili kumwomba wabadili msimamo wa mwongozo huo kwa kuwa utawaathiri wanafunzi wengi ambao ni watoto wa maskini. Hivi karibuni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia walitangaza vigezo vya utoaji mikopo kuwa kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo wapya na wanaoendelea na masomo watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo. Tahliso ilieleza kuwa kutokana na maelezo hayo ni dhahiri mikopo kwa wanafunzi wanaoendelea hasa kwa wale wenye wazazi bila kujali ana uwezo ama hana uwezo, mikopo yao ingepungua kutoka kwenye asilimia walizopangiwa awali. Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa muongozo huo ungepelekea fedha inayotolewa kwa ajili ya chakula na malazi kupungua, jambo ambalo lingesababisha wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo, kutokana na uwezo wa wafamilia wanazotoka hasa watoto wa maskini ambao hutegemea fedha hizo hizo za boom kulipia sehemu ya ada iliyobakia na huku wakiendelea kuishi maisha ya shida vyuoni. Katika vigezo hivyo, Serikali ilisema itatoa kipaumbele kwanza kwa wanafunzi wanaoenda kusomea fani za Sayansi za Tiba na Afya, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia, Sayansi Asilia na Mabadiliko ya Tabianchi na wale watakaosomea Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu. Kwenye vigezo hivyo pia serikali ilisisitiza kuwa kipaumbele kingine kitakuwa ni kwa waombaji hususani wenye mahitaji maalumu kama vile ulemavu na yatima. Seebait.com 2016SeeBait BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APPLICATION MPYA YA MASWAYETU BLOG Share: Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Related Posts: HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA STEFFANO MOSHI MEMORIAL UNIVERSITY 2016/2017 TANGAZO MAALUM KWA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA BUGANDO-CUHAS MWANZA 2016/2017 TAARIFA MUHIMU KUTOKA BODI YA MIKOPO KUHUSU UHAKIKI WA WANAFUNZI UNAFANYIKA UDSM KUANZIA TAREHE 27-29 SEPTEMBA, 2016 MPYA:GAS NA MAJIKO YANAUZWA KWA BEI NAFUU KABISA,UNALETEWA HADI MLANGONI KWAKO MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU SEBASTIAN KOLOWA-SEKOMU DIGRII/BACHELOR 2016/2017 ← Newer Post Older Post → Home Post a Comment Popular Posts MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017 Kama kawaida yetu MASWAYETU BLOG katika nusanusa yetu tumefanikiwa kunasa hii ambayo ilikuwa ikisubiriwa na watu wengi,ni kuhusu ... UPDATED:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA SELECTION YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017 Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa m... MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 10,027 WALIOKOSEA KUJAZA FORM ZA MIKOPO BODI YA MIKOPO 2016/2017 KUONA MAJINA HAYO << BONYEZA HAPA--PDF >> MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017 Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa ma... MPYA:HAYA HAPA MAJINA (KATIKA PDF) WANAFUNZI SPECIAL DIPLOMA WALIOPANGIWA KURUDI UDOM &VYUO VINGINE 2016 >>> CLICK HERE FOR LIST OF SELECTED STUDENT - UDOM (53.28 kB)<<< CLICK HERE FOR LIST OF SELECTED STUDENTS - TEACHER ... ANGALIA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWAPAMOJA NA APPLICATIONS FOR ADMISSION INTO NON DEGREE (DIPLOMA AND CERTIFICATE) PROGRAMMES FOR ACADEMIC YEAR 2016/2017-NACTE Nacte wametoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kuchaguliwa katika vyuo mbalimbali afya,ualimu ,kil... BREAKING NEWS:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO MWAKA WA MASOMO 2016/2017-FIRST BATCH Bodi ya mikopo ya elimu ya juu wametangaza majina ya wanafunzi waliopata mkopo 2016/2017 awamu ya kwanza. Kama utahitaji kuangaliziwa ... MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA SECOND ROUND VYUO VIKUU MBALIMBALI 2016/2017 Habari yako, Maswayetu blog,tumedhamiria kuwapa vitu roho inapenda hapa mjini,Tumeamua kukuwekea list ya vyuo vikuu ambavyo vimetoa ma... MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA CHUO KIKUU UDOM 2016/2017 <<>> BONYEZA HAPA KUONA MAJINA YA VYUO VINGINE ... BREAKING NEWS:HIZI HAPA SIFA ZA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU MWAKA WA MASOMO 2016/2017-TCU Tanzania Commission for Universities PUBLIC NOTICE CHANGE OF PROCEDURES, REQUIREMENTS AND MINIMUM ADMISSION ENT... Recent Posts Text Widget Pages Home Blog Archive ▼ 2016 (2265) ▼ October (180) ▼ Oct 19 (11) MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA ... MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOPATA HOSTE... MPYA:HII HAPA LIST YA VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WA... Zitto Atoa Neno Ugomvi wa RC Arusha na Godbless Le... MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA ... MH.ANTONY MTAKA ATEKELEZA AHADI YA MH.MAGUFULI YA ... Mikopo bilioni 80/- elimu ya juu yapelekwa vyuoni ... MAGAZETI YA LEO JUMATANO OCTOBER 19 2016 Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia ... MPYA:HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI MWAKA WA KWANZA... Mwanafunzi apigwa Dar, ‘afa, afufuka’ mochwari ► Oct 18 (16) ► Oct 17 (7) ► Oct 16 (9) ► Oct 15 (2) ► Oct 14 (4) ► Oct 13 (5) ► Oct 12 (11) ► Oct 11 (8) ► Oct 10 (15) ► Oct 09 (10) ► Oct 08 (10) ► Oct 07 (17) ► Oct 06 (15) ► Oct 05 (14) ► Oct 04 (8) ► Oct 03 (11) ► Oct 02 (5) ► Oct 01 (2) ► September (286) ► August (251) ► July (233) ► June (260) ► May (309) ► April (210) ► March (233) ► February (264) ► January (39) ► 2015 (1416) ► 2014 (1348) ONLINE VISTORS 450 ONLINE

0 comments:

Post a Comment